Moja ya katuni zinazopatikana kwenye machapisho ya fema HIP
BADDHI ya washiriki wa mkutano huo wakiandika mambo yaliyokuwa wakisemwa na viongozi kwenye ufunguzi wa mk
Naibu Waziri wa Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana, Dk. makongoro Mahanga akikabidhi cheti kwa mwakilishi wa klab bora ya Ndanda Sekondari, Ashir Mapunda wakati wa uzinduzi wa mkutano huo.
NAIBU Waziri wa Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana, Dk.Makongoro Mahanga akimkabidhi cheti, balozi mpya wa Fema, Ridhiwani Ridhiwani, wakati wa ufunguzi wa mkutano wa vijana Femina HIP kutoka shule mbalimbali hapa nchini, jana kwenye hoteli ya Belinbda Resort, Kunduchi, Dar es Salaam. Kushoto ni Meneja machapisho wa Fema HIP, Amabilis Matamula na wa pili kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Fema HIP, Minou Fuglesang.
STORY
Naibu Waziri wa Kazi na Maendeleo ya Vijana Dk.Makongoro Mahanga.
Shirika la Vyombo vya Habari Femina HIP, limezindua programu maalum itakayowasaidia vijana pamoja na wanafunzi kuwa wajasiriamali ili kukabiliana na tatizo la ukosefu wa ajira nchini.
Akizindua programu hiyo jana jijini Dar es Salaam, Naibu Waziri wa Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana, Dk. Makongoro Mahanga, alisema programu hiyo itawasaidia vijana kujiajiri wenyewe kutokana na elimu watakayoipata ya ujasiriamali kutoa kwa Femina HIP.
''Serikali kupitia wizara yangu, iko tayari kuendelea kushirikiana na Femina HIP katika juhudi za kutoa mafunzo ya ujasiriamali kwa vijana na uanzishaji wa vyama vya akiba na mikopo ili wapate mitaji ya kuendesha shughuli zao,'' alisema Dk. Mahanga.
Wakati huohuo,Femina HIP imezindua kampeni ya ''haki ya kupata mwanga salama'' yenye lengo la kuelimisha jamii juu ya kutumia nishati mbadala ya kupata mwanga salama.
Akizindua kampeni hiyo Balozi wa Femina HIP 2010, Mrisho Mpoto, alisema lengo la kuanzisha kampeni hiyo ni kuhakikisha Watanzania hususani wanafunzi wanaelimishwa namna ya kujiepusha na majanga ya moto yanayotokea mara kwa mara katika shule za mabweni.
''Watanzania wengi wanatumia mwanga kutoka kwenye taa ambazo si salama zenye kutoa moshi kama mishumaa na taa za mafuta kwa ajili ya matumizi ya nyumbani na shuleni ambazo ni hatari," alisema.
Femina HIP lilianzishwa mwaka 1999 na kauli mbiu ya mwaka huu ni 'Kutoka stadi za maisha hadi kujikimu uhamasishaji wa elimu ya ujasiriamali shuleni.'