Breaking News

Your Ad Spot

Jan 2, 2010

MZEE KAWAWA 'SIMBA WA VITA' AZIKWA DAR,LEO AWAKUTANISHA WATU


Rais Jakaya  Kikwete akisaini kitabu cha Maombolezo alipowasili nyumbani kwa Marehemu Mzee Rashid Kawawa kushiriki katika mzishi yake yaliyofanyika nyumbani Madale nje kidogo ya  jijijni Dar es Salaam leo











Rais Kikwete na viongozi waandamizi wa chama na serikali akiwemo Rais wa Zanzibar Amani Abeid Karume, Makamu wa Rais Dk.Ali Mohamed Sheni, Waziri kiongozi wa SMZ Shamsi Vuai Nahodha wakiuswalia mwili wa marehemu Simba wa vitakabla ua maziko. kijini  Madale nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam, leo. Rais  Kikwete akiweka udongo katika kaburi la marehemu Simba wa Vita, alipoongoza mazishi yaliyofanyika leo, nyumbanbi kwa marehemu , Kijijini  Madale nje kidogo ya  jijini Dar es Salaam.

                            STORI
                                         Suleiman Jongo na Njumai Ngota

VILIO Majonzi na simanzi vilitawala na kusababisha viwanja vya nyumbani kwa Marehemu Simba wa Vita, Mzee Rashid Kawawa, kuzizima wakati wa mazishi ya yaliyofanyika nyumbani hapo, katika kijiji cha Madale nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.

Mazishi hayo yakiongozwa na Rais Jakaya Kikwete, yalihudhuriwa na maelfu ya watu wakiwemo viongozi mbalimbali ndani na nje ya nchi wa serikali na vyama vya siasa.

Shughuli za mazishi hayo zilizanza saa 1.00 asubuhi, kwa kutanguliwa na taratibu za kimila na baadae za kidini kuchukua nafasi ambapo kisomo cha Khitima kilifanyika kikiongozwa na Sheikh wa mkoa wa Dar es Salaam Alhad Mussa Salum.

Mazishi hayo ambayo mbali ya viongozi wa vyama vya siasa kijamii na serikali pia yalishuhudiwa na mabolozi wanaoziwakilisha nchi zao hapa nchini.

Katika hataruki za mazishi hayo mtu mmoja alizimia baada ya kushindwa kuhimili vishindo, ilipogigwa mizinga 19 na Jeshi la Wananchi Wa Tanzania (JWTZ) kwa heshima ya Mzee Kawawa ambaye amepata kuwa Makamu wa Rais na pia Waziori Mkuu wan chi.

Tukio lingine ambalo halikuwa lakawaida, ni pale baadhi ya waombolezaji walistukia wanapiga kofi kumshangilia Mwenyekiti wa CUF, Prof Ibrahim Lipumba, alipokuwa akitoa salamu zauypande wa upinzani na kuonekana kurusha vijembe vya kisiasa.

Eneo lililoonekana kuwagusa watu wengi katika salamu hizo ni pale aliposema moja ya mifano bora ya kujifunza kwa mzee Kawawa ni pamoja na kutulia na kuridhika na chama kimoja badala ya kuhamahama vyama kwa kutafuta maslahi binafsi.

Prof. Lipumba alisema Watanzania hasa viongozi wa siasa wanapaswa kujifunza kutoka kwa mzee Kawawa, uvumilivu na kuridhika kwani wapo baadhi ya viongozi hivi sasa wanaotumia nafasi za uongozi kujilimbikizia mali.

"Ungozi usitumiwe kama sehemu ya ujasiriamali kama mtu anataka kupata mali akafanye shughuli za ujasiriamali zipo nyingi lakini si siasa,” alisema Profesa Lipumba na alipomaliza watu walijisahau kuwa wapo msibani na kupiga makofi kumshangilia.

Maelfu ya watu waliofika Madale kwa mazishi hayo walisababisha walifanya eneo la nyumba ya marehemu mzee Kawawa kuwa dogo na kulazimika wengine kuzuiwa kuingia katika uzio wa kwa sababu za kiusalama.

Katika mazishi hayo ambayo pia yalifanyika kwa taratibu za kiserikali, makundi ya kada mbalimbali kijamii, kisiasa na kiserikali, yalipata fursa ya kutoa salamu na kueleza wanavyo mkumbuka marehemu mzee Kawawa.

Salamu za kwanza zilitoka katika kundi la marafiki lililowakilishwa na mzee George Kahama, aliyemwelezea marehemu Kawawa kama kiongozi wa kuigwa katika taifa hili.

Mzee Kahama alisema nyota ya mzee ya uongozi bora wa mzee Kawawa ilianza kuonekana tangu walipokuwa shule ya sekondari ya Tabora Boys mwaka kwani alikuwa mtulivu msikivu na kumvuta kla mmoja shyleni hapo.

“Hata mwali Julius Nyerere alipomteua kuwa Waziri Mkuu katika baraza letu la mawaziri kila mmoja aliridhika na uteuzi huo,” alisema Mzee Kahama.

Katika mazishi hayo mizinga 19 ilipigwa ikiwa ni ishara ya kumuaga marehemu mzee Kawawa.

Mbali ya mizinga hiyo pia kikosi cha maombolezo cha Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), kiliendesha gwaride rasmi la kumuaga mzee Kawawa.

Pia kikundi hicho kilipiga wimbo wa Taifa mara kabla ya kulibeba jeneza tayari kwa kulipeleka makubulini, walipolifikisha jeneza na baada ya kumzika walipiga wimbo wa taifa ikiwa ni utaratibu wa kijeshi.

Mazishi hayo pia yalishuhudiwa na nchi marafiki wa Tanzania ambazo mzee Kawawa alishiriki kwa kiasi kikubwa kuzipatia uhuru.

Katika salamu za kwenye mazishi hayo, ujumbe wa serikali na chama cha FRERIMO cha nchini Msumbiji zilizosomwa na Jenerali Mstaafu Raymund Domingo alisema Rais Armando Guebuza na wananchi wa Msumbiji wameguswa na kifo hicho.

Domingo alisema watamkumkumbuka mzee Kawawa kutokana na mchango wake mkubwa alioutoa walipokuwa wakipigania uhuru wan chi yao ambapo alishirikiana na hayati mwalimu Juliu Nyerere kuhakikisha harakati hizo zinatimia.

Kwa upande wa ujumbe kutoka nchini Uganda uliowasilishwa na Naibu Waziri Mkuu wa nchi hiyo Elia Kategaye, alisema walikuwa wapo katika harakati za kutaka kumualika aende nchini humo na kumpongeza kwa mchango wake wakati wa mapambano na dikteta Nduli Idd Amin.

Kwa mujibu wa Kategaye, mwaka 1972 Mzee Kawawa aliwapa paundi 50,000 kama sehemu ya maandalizi ya mapambano.

Hata hivyo katika wengi panakuwa na mengi wakati watu wengi waliofika katika mazishi hayo wakishughulika na mazishi mwanamke mmoja ambaye hakufahamika jina alikamatwa an kutolewa nje ya uzio wa nyumba baada ya kukutwa akiwa ameeba simu ya mkononi kutoka kwa jirani yake.

Akiwasilisha salamu kutoka serikali ya mapinduzi ya Zanzibar wa Waziri wa Utawala Bora wa Zanzibar Ramadhan Shaban Abdallah, alisema kifo cha mwanasiasa huyo kitaacha pengo kubwa nchini.

Abdallah alisema mzee Kawawa alipigania mapinduzi ya Zanzibar akishirikiana na haya Nyerere na mzee Aanani Aabeid Karume, hivyo kitu pekee cha kufanya ni kuyaenzi yale yote aliyoyapigania.

CIAO












Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages