Breaking News

Your Ad Spot

Feb 3, 2010

AJALI YA BASI YAU 22, KUJERUHI 37 TANGA

WATU 22 wamekufa papo hapo na wengine 37 kujeruhiwa, katika ajali iliyotokea wilayani Handeni, Tanga.

Ajali hiyo imehusisha basi la kampuni ya Chatco lililogongana uso kwa uso na basi dogo liitwalo Nzuri.

Mkuu wa Upelelezi mkoa wa Tanga, Jaffar Mohammed, alisema ajali hiyo ilitokea jana saa nane mchana katika kijiji cha Kitumbi Kwamgolo, wilayani Handeni.

Alisema ajali hiyo ilihusisha basi la Chatco lenye namba za usajili T 548 ANC lililokuwa likitokea Arusha kwenda Dar es Salaam na basi dogo lenye namba T 602 AMU. Kwa mujibu wa Mohammed, chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi wa basi dogo.

Watu walioshuhudia ajali hiyo walisema ilitokea wakati basi hilo dogo lilipokuwa likijaribu kulipita lori.

Mohammed alisema majeruhi wa ajali hiyo walipelekwa katika Hospitali ya Magunga, wilayani Korogwe na Hospitali Teule ya wilaya ya Muheza. Alisema dereva wa Chatco, aliyetajwa kuwa Mambo Mlamwa, alitoroka baada ya ajali na polisi wanaendelea kumsaka.

Kwa mujibu wa Mohammed, miili ya watu waliokufa imehifadhiwa katika Hospitali ya Mkoa wa Tanga ya Bombo. Hii ni ajali kubwa ya kwanza kutokea mkoani Tanga tangu kuanza kwa mwaka huu. Mwaka jana zilitokea ajali mbili kubwa, ikiwemo ya basi la kampuni ya Mohamed Trans lililosababisha vifo vya watu 28. Nyingine ya basi la Tashriff liliua watu 27.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages