Christian Bella, Rais wa Akudo Impact
WANAMUZIKI ambao ni waimbaji wapaya wa Akudo Impact
STORI
BAADA ya kutamba na albamu ya kwanza ya Impact mwaka juzi na mwaka leo, bendi ya Akudo Impanct imesema imeandaa albamu ya pili ambayo imedai itakuwa mto wa kuopteaa mbali kuliko ya kwanza.
Akizungumza na waandishi wa habari leo, Mkurugenzi wa bendi hiyo, Miuchael Loki alisema, nyimbo mbili kati ya nane zitakazokuwa katika albamu hiyo zimekamilika.alisema, albamu hiyo ambayo imepewa jina la 'History no Change'itaakuwa mitaani na katika vituo vya radio na televisheni hivi hivi karibuni.
Rais wa bendi hiyto Christian Bella, alitaja nyimbo zilizopo tayari kuwa ni aliotunga wa 'Pongenzi kwa wenye ndoa' na 'ubinafsi uliotungwa na Tarsisi Masela. Alisema, nyimbo nyinginebado ni siri ukiwemo History No Change ambao umebeba albamu hiyo aliosema kwamba hangeweza kutaja mistari yake kwa waandishi wa habari kwa kuwa nfiyo silaha itakayomtoa nyoka pangoni. Bella alitamba kwamba pamoja na kwamba albamu ya Impact haikutumika sana kuingiza pato la bendi hiyo katika mauzo lakini ilifanya kazi kubwa ya kuifanya bendi ishike kwa wamashabiki.
Alisema kazi ya albamu mpya itakuwa ile ile ya kuiweka juu Akudo na kuifanya izidi kupendwa zaidi na
zaidi na mashabiki. Bella alisema, pamoja na katika kufyatua albamu hiyo mpya, Akudo pia imeleta waimbaji wapya watatu kutola Jamhuri ya Kimokrasi ya Congo aliowataja kuwa ni Kabaston Mwanamulenda, Alain Frapa na Fredy Panzu.
Albamu ya Impact ilikuwa na nyimbo kadhaa lakini ulioonyesha kutia fora ni 'Yako wapi Mapenzi' uliotungwa na Bella.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269