Breaking News

Your Ad Spot

Feb 6, 2010

KILELE CHA MIAKA 33 YA CCM YALIYOFANYIKA MNAZI MMOJA, JIJINI DAR LEO

                              HABARI KATIKA PICHA
MWENYEKITI wa CCM Rais Jakaya Kikwete akifurahia gwaride la Chupikizi wa CCM lililofanyika katika kilele cha maadhimisho hayo, leo. Wengine ni Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Pius Msekwa, Katibu Mkuu wa CCM Yussuf Makamba, Mama Salma Kikwete na Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara), George Mkuchika.Vijana wa CCM wakitoa heshima mbele ya Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete wakati wa gwaride lao katika kilele hicho
Vijana wa Chipukizi wa CCM, wakitoa heshima kwa Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Kikwete katika gwaride waliloshiriki kwenye kilele hicho.
MWENYEKITI wa CCM Rais Jakaya Kikwete akiuongoza wana-CCM waliohudhuria kilele hicho kusimama kwa muda kama ishara ya kumbukuka Mwasisi wa CCM, Mzee Raishid Kawawa aliyefariki dunia Desemba 31 mwaka jana
.
Kikundi cha Tanzania One Theatre (TOT Plus) likitumbuiza katika kilele cha sherehe hizo.
KATIBU Mkuu wa CCM Yussuf makamba akimkaribisha JK kuhutubia wakati wa kilele hicho.
WANAMUZIKI wa bendi ya Vijana wakiimba wimbo maalum katika kilele hicho
BAADHI ya makada wa CCM waliohudhuria sherehe za kilele cha maadhimisho hayo.

BAADHI ya viongozi wa ngazi mbalimbali za CCM na Umoja wa VIjana wa CCM wakiwa kwenye sherehe za kilele hicho.
BAADHI yua waandishi wa habari kutoka UHURU FM na UHURU, Mzalendo na Burudani wakibadilishana mawazo kwenye sherehe hizo.
WASANII wa kikundi cha Fataki wakiburudisha
JK akicheza wimbo wa TOT Plus kabla ya kuhutubia kwenye kilele hicho.
=============================
MSANII ALIYENG'ARA KWENYE SHEREHE HIZO
VICKY KAMATA
VICKY akibadilishana mawazo na Mkurugenzi wa TOT Plus,kapteni John Komba kabla ya kupata fursa ya kutumbuiza kwenye kilelecha maadhumisho hayo ya miaka 33 ya CCM 
AKIIMBA wimbo wake wa 'Hongera CCM' ambao ulivutia wengi
VAI Mzindakaya ambaye ni mmoja wa viongozi waandamizi wa CCM, akimtuza Vicky kwa kumpachika usoni noti ya sh. 10,000.
====================================
MTOTO ALIYENG'ARA
 
SOPHIE Furaha Luhende (7) ambaye ni mtoto wa mfanyakazi wa UHURU FM, Furaha Luhende ni miongoni mwa watoto walioonyesha mvuto kwa watu mbalimbali waliohudhuria sherehe za kilele hicho akiwemo Mwenyekiti wa CCM, Rais Kikwete.
MVUTO wake ulitokana na alivyopambwa mavazi ya ki-CCM na kuvaa kichwani utepe ulioonyesha CCM kutimiza miaka 33.
Sophie akiwa katika pozi na ofisa Uhusiano wa Benki Kuu ya Tanzania, ambaye pia ni mwanamuziki na kada wa CCM, Vicky Kamata ambaye inaonekana pia alivutiwa kuwa na mtoto huyo.MKURUGENZI wa TOT Plus, John Komba akiwa na Sophie kwenye sherehe hizo ambaye naye ni miongoni waliobutiwa naye.
Sophie akiwa amepimzika ka kiongozi wa CCM Vai Mzindakaya kwenye sherehe hizo
RAIS Jakaya Kikwete akimuuliza jambo baada ya kumuona wakati akiondokakatika baada ya sherehe hizo.
RAIS Kikwete akimsalimia baba wa mtoto huyo, Furaha Luhende baada ya kutambulishwa kwa Rais  na mtoto huyo.
JK akiendelea kuonyesha hamu ya kuwa na mtoto huyo, huku Vai Mzindakaya naye akiwa pembeni.

MKUU WA VIPINDI UHURU FM, ANGEL AKILIMALI HAKUWA NYUMA !
MKUU wa vipindi UHURU FM Angel Akilimali ambaye pia ni Mkumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM, akitoka kwenye sherehe hizo  huku akiwa katika suti zake za kijani zilizotawalasiku hiyo
Angel Akilimali
Angel akimwaga cheko kufurahia shamshara za kilele cha maadhimsho hayo.
Angel akisoma gazeti la UHURU baada ya kupita katika ofisi za uchapishaji wa gazeti hilo za Uhuru Publications Ltd, mtaa wa Lumumba, Dar es Salaam, baada ya kutoka viwanja vya Mnazi Mmoja kwenye sherehe hizo

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages