Reginard Mengi
STORI
UVUMI ulionezwa jijini Dar es Salaam, kuhusu mwanamke kuota manyoa baada ya kumpa msaada mlemavu, umeelezwa kuwaathiri walemavu.
Hayo yalisemwa na Mwenkiti wa Kampuni za IPP, Reginald Mengi katika mkutnao wake na waandishi wa habari, jana mjini Dar es Salaam.Mengi alisema, uchunguzi aliofanya tangu uvumi huo ulipoenezwa na baadhi ya vyombo vya habari na watu mbalimbali, jijini walemavu kadhaa wamekosa amani na kutoweka katika maeneo walikokuwa wakikaa kusubiri misaada kwa wapitanjia.
Alisema, mbali na kuwaweka katika mazingira magumu ombaomba wanaoendesha maisha yao kwa njia hiyo, hata wengine wenye ulemavu ambao hawaishi kwa kuomba omba wameonekana kudhalilika kutokana na uvumi huo.
Mengi alisema, wenye ulemavu sasa wanajisikia kama tabaka lingine la binadamau kwa kuwa uvumi huo umewafanya kuonekana kama mlemavu ni aina fulani ya jinamizi au jini jambo ambalo ni hatari.
Alisema, kama uvumi huo ulilenga kutaka wenye ulemavu wajitegemee imekuwa kinyume, kwa sababu sasa hata wale waliokuwa na shughuli zao ndogo ndogo za kuwaingizia kipato kama kuuza vocha za simu na wanakosa wateja kwa sababu yakihofiwa kuwa siyo watu wa kawaida.
Aliviomba vyombo vya habari vilivyosaidia kuenea uvumi huo, kutumia nguvu ilele ile au zaidi kuielimisha jamii kuwa jambo hilo halikuwa kweli na bado walemavu ni sehemu ya jamii.
Wiki iliyopita, ulisambaa uvumi katika jiji la Dar e Salaam na viunga vyake, kwamba kulikuwa na mwanamke ambaye aliposimamisha gari lake kusubiri taa, alimpa fedha ombaomba eneo la Selander Bridge, na ghafla akaota manyoa mkononi.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269