BAADA ya miaka zaidi ya 15, tangu Mwenyekiti wa TLP,Augustine Mrema (Pichani) aachie ngazi kutoka CCM na kutimkia NCCR Mageuzi, sasa leo ameiomba serikali kumkumbuka na kumpatia mafao kwa nyadhifa za Unaibu waziri Mkuu na Uwaziri wa mambo ya Ndani alizowahi kutingisha nazo.
Mrema Alisema hayo leo katika mkutano na waandishi wa habari makao makuu ya chama hicho yaliyopo Magomeni Dar es salaam.
Alisema pamoja na kuwa alipoteza mafao yake alihamia chama NCCR-Mageuzi mwaka 1995 anapaswa kulipwa kwakuwa alitoa mchango mkubwa kwa taifa.
Mrema alikuwa akizungumzia madai kuwa alienda nchini India kutibiwa ugonjwa wa Kisukari kwa gharama za Rais Jakaya Kikwete, madai ambayo alikanusha vikali.
Alisema alikwenda India kwa gharama zake mwenyewe hakulipiwa na TLP wala mtu yeyote nakuwataka waandishi wa habari wasiandike habari za kumdhalilisha kwakuwa hajafikia hatua ya kushindwa kujilipia gharama za matibabu.
"Jamani kwanini mnanidhalilisha hivyo, ina maana hata gharama za matibabu yangu hapo India nimeshindwa kujilipia?, kuna nini mpaka mjadili afya yangu" alihoji Mrema.
Aliongeza: Fadhila za matibabu itanisadia nini, kama kuna uwezekano naomba serikali inilipe mafao yangu niliyonyimwa baada ya kujiunga NCCR-Mageuzi.
"Ni haki yangu ile, mbona Maalim Seif amepewa na alikuwa na kesi ya kuhujumu uchumi, nimefanya nini kibaya katika nchi hii mpaka ninyimwe mafao yangu jamani" alihoji Mrema.
Hata hivyo alisema ataendelea kumtetea Rais jakaya Kikwete dhidi ya hujuma anazofanyiwa na endapo atashinda Ubunge wa jimbo la Vunjo mkoani Kilimanjaro atafanya naye kazi.
Your Ad Spot
Feb 1, 2010
Home
Unlabelled
MREMA ATOKA KUTIBIWA INDIA, AKUKUMBUKA MAFAO YA UNAIBU WAZIRI MKUU ALIOUTEMA ZAIDI YA MIAKA 15 ILIYOPITA
MREMA ATOKA KUTIBIWA INDIA, AKUKUMBUKA MAFAO YA UNAIBU WAZIRI MKUU ALIOUTEMA ZAIDI YA MIAKA 15 ILIYOPITA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Top Ad
Your Ad Spot
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269