Chuo Kikuu cha Fatih cha nchini Uturuki kinatarajiwa kumtunuku Rais Jakaya Kikwete, Shahada ya Uzamivu (PhD) ya heshima, imefahamika.
Ikulu, Dar es Salaam imesema, Rais Kikwete ameondoka jana nchini kwenda Uturuki na pia atakwenda Jordan, kwa ziara rasmi za kiserikali kwa mwaliko wa viongozi wa nchi hizo.
Rais Kikwete anafuatana na mkewe, Mama Salma, pamoja na wafanyabiashara wa Tanzania.
Atafanya ziara ya siku tatu nchini Uturuki kwa mwaliko wa Rais Abdallah Gul. Alipokea na kukubali mwaliko wa kuitembelea Uturuki Februari mwaka jana wakati Rais Gul alipotembelea nchini kwa mwaliko wa Rais Kikwete.
Atakapokuwa Uturuki, Rais Kikwete atazungumza na mwenyeji wake na pia kukutana na kuzungumza na Waziri Mkuu wa Uturuki, Recep Tayyip Erdogan.
Rais Kikwete pia anatarajiwa kuzungumza na viongozi wa Chama cha Wafanyabiashara wa Uturuki na mabalozi wa Afrika wanaowakilisha nchi zao nchini humo.
Tanzania na Uturuki zinatarajiwa kusaini mikataba sita ya ushirikiano. Rais anatarajiwa kuondoka Uturuki Jumapili, kwenda Jordan kwa ziara ya siku tatu kwa mwaliko wa Mfalme Abdullah II.
Your Ad Spot
Feb 18, 2010
Home
Unlabelled
RAIS KIKWETE KUTUNUKIWA PHD UTURUKI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Top Ad
Your Ad Spot
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269