Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova akionyesha leo pingu inayodaiwa kukutwa katika gari la Mtangazaji wa TBC1, Jerry Murro aliupokamatwa juzi, awali akituhumiwa kuomba rushwa kwa vitisho.
STORY
Kamanda wa Polisi Kanda maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova leo amezungumzia skata la kukamatwa na kuhojiwa Mtangazaji wa TBC 1 Jerry Murro, kuhusu madai ya kudai kwa vitisho rushwa ya sh. milioni 10 kutoka kwa mkazi wa jijini Dar es Salaam, Michael Carlos aliyekuwa mhasibu wa Halmashauri ya Mji wa Bagamoyo kabla ya kutemeshwa mzigo na Waziri Mkuu Mizengo Pinda hivi karibuni.
Akizungumza na waandishi wa habari leo, Kova amesema Carlos alitoa taarifa polisi akidai kuna watu wanamsumbua sana na kumtisha wakidai awape sh. milioni 10 kabla ya kuibua kashfa zake kwenye vyombo vya habari, hivyo Kova aliwaamuru vijana wake kufuatilia tukio hilo katika mgahawa wa City Garden jijini na kuikuta gari ikiwa imeegeshwa , ilibidi Michael awasiliane na huyo mtu ili waingie hapo hotelini hata hivyo huyo mtu huyo alikataa na hivyo wakamfuata kwenye gari lake na kukuta ni Muro.
Anasema walimchukua mpaka kituo cha polisi na kuchukua maelezo ya bwana Michael ambaye alisema anamfahamu Jerry Muro kwani wamekuwa wakikutana katika maeneo kadhaa jijini, pia akadai kwamba kuna miwani yake aliisahau kwenye gari ya Jerry Murro na pia kuna pingu na Silaha yaani bastola ambvyo mtuhumiwa huyo alikuwa akitumia kumtishia ili atoe hizo fedha.
Hata hivyo Kova hakuthibitisha kama Murro amekamatwa na hizo sh. milioni 10, lakini amesema kujipatia fedha au kumdai fedha mtu yeyote kwa kumtishia ni kosa la jinai, hivyo kutokana na mazingira ya maelezo ya mlalamikaji na vielelezo vinatufanya kuamini kwamba tukio hilo lilikuwepo, ameongeza kuwa hawakuweza kuwashirikisha PCCB katika mtego huo kwakuwa muda ulikuwa ni mdogo na mtuhumiwa angeweza kukimbia na kuwapotea
Kuhusu Bastola ambayo inamilikiwa na Jerry Murro, Kova amesema silaha hiyo imetengenezwa nchini Chec. Repumlic ni SZ 97 B NO A 6466 inayobeba risasi 10 anaimiliki kihalali kabisa, ina vibali vyote na alipewa kwa ajili ya kujilinda na maadui zake kutokana na kazi zake za habari za uchunguzi, Isipokuwa pingu ambazo hakuna raia ambaye anaruhusiwa kumiliki kisheria
Ameongeza kwamba kesi hiyo wataipeleka kwa mwanasheria wa Serikali ili aone kama kuna kesi ya kujibu na kuipeleka mahakamani ili haki itendeke kwa kila upande na kama itakuwa vinginevyo watamuita bwana Maiko Calos ambaye ni mlalamikaji na kumwambia yaliyojiri kutoka kwa mwanasheria wa Serikali.
Muro ambaye alikamatwa jana, na kusababisha vuguvugu lakusambaa kwa taarifa hizo nchini, hadi leo alikuwa nje kjwa dhamana.
MURO akionyesha nyarakambalimbali zikiwemo za uhalali wa kumiliki bastola,alipokuwa kwenye kituo kikuu cha polisi jijini Dar es salaam jana.
KATIKA HATUA NYINGINE
BARAZA la Habari Tanzania (MCT) limesema litamtetea mwandishi wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Jerry Muro, ambaye anatuhumiwa kwa kudai rushwa na kuwataka waandishi wengine kuendelea na kuendelea na kazi bila woga.
Akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za Baraza hilo, Dar es Salaam jana, Katibu Mkuu wa MCT, Kajubi Mukajanga, alisema pamoja na tuhuma hizo, Muro bado ni mwandishi wa kupigiwa mfano kwani kazi zake za kufichua maovu zimeonekana nchini.
Alisema tuhuma hizo ni njama za kutaka kuwanyamazisha waandishi wa habari ambao wamekuwa wakifanya kazi nzuri na si jambo la kushangazwa kuona tukio hilo limetokea.“Tunafahamu kwamba Jerry alikuwa
anafanya habari ya uchunguzi inayohusisha vigogo wakiwemo mawaziri, ambayo iko mbioni kurushwa, hii ni njama ya kutaka kudhoofisha kazi zake,” alisema Mukajanga na kuongeza kuwa, baraza halitakuwa tayari kuona hali hii inaendelea.
Alilitaka jeshi la polisi kufanya uchunguzi wa haraka kuhusiana na suala hilo na kulifikisha mahakamani kama tuhuma hizo zikipatiwa ushahidi ili mahakama iweze kuweka bayana. “Ni kawaida siyo kwa Tanzania tu,
waandishi wamekuwa wakipata vitisho, vipigo na mara nyingine kuuawa hasa wale wanaofanya habari za uchunguzi,” alisema Mukajanga na kuongeza kuwa ndiyo maana kumekuwepo na mfuko maalumu kwa ajili ya kuwatetea waandishi wanaopata matatizo ya aina hiyo.
Alisema mazingira ya tuhuma hizo yanatatanisha na kuwataka polisi kufanya kazi wa weledi na kuacha
kuwatisha wengine wawapo kazini. “Bastola walimpa wenyewe na anamiliki kihalali…Jerry hana kosa hadi
mahakama itakapoamua,” alisisitiza.
Mukajanga aliwataka waandishi wa habari kuwa makini na kuonya kuwa wataendelea kuandamwa hususan katika kipindi hiki kinachokaribia uchaguzi mkuu. “Huu ni mwaka wa uchaguzi, pamoja na kuwataka mfanye kazi nzuri, mnapaswa kuwa waangalifu, kwani vitendo kama hiivyo, " alisema Mukajanga.
MCT imetoa kauli hiyo ikiwa ni siku moja baada ya Muro kutiwa mbaroni na kuhojiwa na polisi kuhusiana na tuhuma za kudai rushwa. Hata hivyo aliachiwa kwa dhamana.
CIAO
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269