KATIBU Msaidizi mkuu daraja la II,Idara ya Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi(CCM),Akwilombe Shaib Ally jana ametangaza rasmi kugombea ubunge jimbo la Tunduru Kaskazini.
Akwilombe alitangaza nia hiyo wakati akizungumza na gazeti hili kwenye ofisi ya CCM Lumumba mjini Dar es Salaam kwamba amepanga kufanya hivyo baada ya kuombwa na wakazi wa eneo hilo.
Alifafanua kuwa amekubali maombi hayo ya wakazi wa eneo hilo ingawa bado mipaka ya kugawa jimbo hilo inaendelea na kutokea majimbo mawili ya Kusini na Kaskazini.
Akwilombe alieleza kuwa ameamua kufanya hivyo kutokana na kufahamu vilivyo changamoto ya jimbo hilo hasa kutaka kuwaunganisha viongozi,wanachama wa CCM kuwa kitu kimoja.
Alisema kwamba lengo la kufanya hivyo ni kutaka kuhakikisha Chama kinakuwa na umoja ili kuweza kuwashinda wapinzani katika uchaguzi ujao,Oktoba mwaka huu.
"Najua pale kuna mgawanyiko,wazee,vijana wamenifuata kutaka kugombea nafasi hiyo,nami nilifikiri kwa mapana na marefu na kuamua kukubali"alisema Akwilombe.
Mgombea huyo alisema kuwa sambamba na kuhimiza umoja pia akipata nafasi hiyo anataka kurejesha ushirikiano na serikali kuwapa maendeleo wananchi wa jimbo hilo.
Kama Tume ya uchaguzi itafanikisha kugawa jimbo hilo,Kaskazini itakuwa ipo katika mji wa Tunduru na tarafa ya Matemanga ambapo atahakikisha mji huo unakuwa na taswira ya maendeleo.
Aidha alisema kuwa ana lengo la kuhakikisha kuwa wakazi wa mji huo wanapata huduma muhimu kama maji,hospitali na nyinginezo ambazo kwa sasa zipo ingawa bado hajakidhi matatizo yote ya wananchi.
"Nimejipanga kuhakikisha nikipata nafasi hiyo,ninawaletea maendeleo wananchi wa jimbo kwa kushirikiana na serikali ya ambayo itaundwa na CCM,nina hakika CCMitaendelea kuongoza nchi"alisema mgombea huyo.
Your Ad Spot
Apr 23, 2010
Home
Unlabelled
AKWILOMBE ATAKA UBUNGE TUNDURU
AKWILOMBE ATAKA UBUNGE TUNDURU
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Top Ad
Your Ad Spot
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269