B, kwenda Chuoni.
Baada ya wanafunzi hao kutelemka, Bashir aliiona simu hiyo ikiwa kwenye siti na kuiokota na kisha kuihifadhi bila kuizima hadi alipopigiwa na mwanafunzi huyo kupitia simu ya rafiki yake Doris Valentine (wapili kulia) baada ya nusu saa hivi tangu washuke.
Bashir alipokea simu na kumhakikishia Julieth kuwa asiwe na wasiwasi atamtunzia simu hiyo hadi kumkabidhi.
Baada ya kuhakikishiwa atapata simu yake, mwanafunzi huyo aliomba Bashir amtunzie bila kuizima simu hiyo, yeye anakwenda kufanya mitihani kwanza chuoni na atamtafuta baadaye.
Kiasi cha saa 6 mchana, Jully alipiga tena simu mawasiliano ndipoendelea hadi walipokutana kwenye jengo hilo na kumkabidhi simu hiyo ambapo Jully alionekana kufurahi zaidi na kutoamini imani ya Bashir jambo lililomfanya kubaki akimkodolea macho mara mbilimbili.
Je una maoni gani kuhusu tukio hili?
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269