Timu tatu nyingine zilizokabidhiwa ni za mikoa ya kisoka ya Ilala, Temeke, na Kinondoni.
Akizungumza katika hafla hiyo iliyofanyika katika ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam , Meneja Matukio wa TBL Zozimick Kimati alisema kuwa wanajivunia kuendelea kudhamini mashindano hayo ambayo ni ya pili kwa ukubwa hapa nchini ili kuhakikisha soka la Tanzania linasonga mbele.
Katika hatua nyingine mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam William Lukuvi alikabidhi kiasi cha sh milioni 1.5 kwa kila timu na kuishukuru TBL kwa msaada hguo.
”Tunawapongeza TBL kwa mchango wao katika maendeleo ya soka la Tanzania,” alisema Lukuvi na kuyaomba makampuni mengine yawe mstari wa mbele kuchangia katika michezo.
TBL imekabidhi shilingi milioni 1.5 kwa kila timu itakayoshiriki katika mashindano haya na kugharamia hela ya malazi, chakula na usafiri. Jumla ya timu zinazoshiriki ni 24.
Kampuni hiyo imedhamini mashindano kwa jumla ya zaidi ya shilingi miloni 850 kama ufadhili mzima ambapo mshindi wa kwanza atajinyakulia kitita cha sh 35 milioni wakati mshindi wa pili atachukua shilingi milioni 20, wa tatu atapata shilingi milioni 10 na wanne atapata shilingi milioni 5.
Michuano hiyo inatarajiwa kutimua vumbi Jumamosi Mei 8, 2010 katika vituo vya Mwanza, Tanga, Arusha, Iringa, Dodoma na Mtwara kwa hatua za awali na watakaofuzu watasafri Dar es Salaam kwa hatua ya robo fainali, nusu fainali na kisha fainali ambayo inatarajiwa kupigwa Mei 29, 2010.Hii ni mara ya nne mfululizo kwa TBL kudhamini mashindano haya na ni mara ya pili kwa kinywaji cha Kilimanjaro Premium Lager.
HABARI KATIKA PICHA
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, William Lukuvi (kushoto) akikabidhi fedha za maandalizi kwaajili ya timu ya Mkoa wa Temeke Shilingi Milioni 1.5 kwa Katibu Mkuu wa Chama cha Mpira wa Miguu Temeke (TEFA) Bakili Bakele (kulia) katikati ni Meneja Matukio wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) Zozimick Kimati.Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, William Lukuvi (kushoto) akikabidhi fedha za maandalizi kwaajili ya timu ya Mkoa wa Temeke Shilingi Milioni 1.5 kwa Katibu Mkuu wa Chama cha Mpira wa Miguu KINONDONI (KIFA) Frank Mchaki (kulia) katikati ni Meneja Matukio wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) Zozimick Kimati.Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, William Lukuvi (kushoto) akikabidhi fedha za maandalizi kwaajili ya timu ya Mkoa wa Temeke Shilingi Milioni 1.5 kwa Katibu Msaidizi wa Chama cha Mpira wa Miguu Ilala (IDFA) DAUDI Kanuti (kulia) katikati ni Meneja Matukio wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) Zozimick Kimati. (PICHA ZOTE NA EXECUTIVE SOLUTIONS).
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269