BAADA ya kusota mwaka mmoja rumande, wakati kesi yake kuhusu matumizi mabaya ya ofisi na kuitia hasara serikali, aliyekuwa Meneja Utawala na Utumishi wa Benki Kuu ya Tanzania, Amatus Liyumba, leo amehukumiwa kifungo cha miaka miwili jela, sawa na miezi 24.
Kulingana na taratibu wa vifungo hapa nchini, miezi hiyo 24 itahesabiwa kwa usiku na mchana, hivyo atatumikia jela hadi Mei Mwakani, huku uwezekano wa kutoka mapema kwa msamaha wa rais ukiwa wazi kwa kuwa kosa lililomtia hatiani si katika makosa ambayo hayaruhusu kupata msamaha wa Rais yakiwemo ya ubakaji, uhujumu uchumi na kupatikana na dawa za kulevya.
Baada ya kuhukumiwa katika mahakama ya Kisutu jijini Dar es Salaam, Wakili wa Liyumba , Magafu amesema atakata rufani.
Habari katika Picha
Basi la magereza likiwasili na Liyumba mahakama ya KisutuLiyumba akishukaAkisindikizwa na askari magereza kwenda kizimbaniLiyumba akiingia chumba cha mahakamaAkiwa katika benchi kabla ya kupanda kizimbaniLiyumba akipewa ufafanuzi na wakili wake Majira Magafu (kushoto) baada ya hakimu kumtia hatiani na kutoa mapumziko ya nusu saa kabla ya kutoa adhabu.Liyumba akisindikizwa na askari magereza baada ya hukumuMTU mmoja mwenye nywele za kusokotwa maarufu kama rasta, akijifatagua kwa kuonyesha alama ya vodole viwili mbele ya Liyumba aliyekuwa akipelekwa rumande ya mahakama kabla ya kwenda jela.Mahakama ikiwa imefurika watu, wengi wao wakiwa ni ndugu na jamaa.Liyumba akiwa chini ya ulinzi wa askari magereza baada ya hukumu
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269