Hatimaye Makamu wa Rais, Dk Ali Mohammed Sheni amepita kuwa mgombea Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CCM, katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba mwaka huu baada ya kuchaguliwa kwa kura 117 na kuaacha mbali waziri Kiongozi mstaafu Dk. Mohamed Gharib Bilal aliyepata kura 54 na waziri Kiongozi wa sasa, Shamsi Vuai Nahodha aliyepata kura 33, katika uchaguzi wa kinyang'anyiro hicho uliofanywa na wajumbe wa Mkutano Mkuu wa taifa (NEC) ya CCM jana usiku katika ukumbi wa Kizota mjini Dodoma.
Dk. Sheni amepenya baada ya kuingia wakiwa watatu waliopenya awali katika mchujo wa Kamati Kuu wa CCM lakini akiwa pia katika wale watano waliokuwaa wamependekezwa na Kamati maalum Zanzibar, kati ya jumla ya makada 11 waliochukua fomu na kuzirejesha kuwania nafasi hiyo inayoachwa ana rais wa sasa Amani Abeid Karume.Dk Ali Mohammed Sheni akizungumza baada ya kuchaguliwa
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269