Breaking News

Your Ad Spot

Jul 8, 2010

MAELFU WAKOSA FIESTA MORO BAADA YA TIKETI KUISHA

*Waandaaji walikadiriwa tiketi 20,000, lakini zikaisha
*Wakauza hadi vishina lakini watu wakawa bado nyomi nje
TAMASHA la Fiesta mwaka huu limeanza kwa kishindo baada ya onyesho lake la kwanza lililofanyika katika Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro kufurika maelfu ya watu huku mamie wengine washindwa kuingia kutokana na kumalizika tiketi.

      Hadi kufikia saa 12 jioni uwanja ulikuwa umefurika maelfu ya watu wengi wao wakiwa ni vijana na watoto, na mamia ya watu wengine walibaki wakisikilizia nje baada ya kushindwa kuingia licha ya kwamba walikuwa na fedha za kiingilio.
      Mkurugenzi wa Prime Time Promotions, Ruge Mtahaba alisema, idadi ya tiketi zilizokuwa zimekadiriwa zilimalizika, hadi wakalazimika kuuza hadi vishina vya tiketi walizouza awali lakini bado mamia ya watu waliendelea kujazana mlangoni wakitaka tiketi.
      Onyesho lilianza saa 8 mchana kwa wasanii mbalimbali wa mjini Morogoro, kutoa burudani, hadai saa 1.30 onyesho lilipoanza rasmi kwa kupaanda wasanii mahiri waliopagawisha mashabiki vilivyo.
      Wasanii hao ni Joe makini, Fid Q, kundi la Tip Top Connection kutoka Manzese, Mwana FA, kundi zima la THT, Kalapina, Diamond, B elle 9, Mwasiti, Hussein Machozi Godzila, Jcb, Juma Nature, Chege na Temba.
      THT ndiyo walionyesha kukonga zaidi nyoyo za mashabiki, baada ya kuonyesha umahiri wao walipopanda jukwaani na kulisakata vilivyo sebene linalotamaba katika anga la muziki hapa nchini la 'Ala G'.
     "sasa hapa kiingilio chetu kimekwenda kihalali, maana vijana hawa wanajituma si mchezo", alisikika shabiki mmoja aliyekuwa miongoni mwa maelfu ya mashabiki waliokuwa wakaishangilia THT walipomaliza 'kukamua'.
     Baada ya fungua dimba kwa onyesho hilo, maonyesho mengine la Fiesta inaroratibiwa na kampuni ya Prime Time Ptomotions na kudhaminiwa na bia ya Serengeti, yatarindima katika mikoa mingine ikiwemo ya Arusha, Mwanza na Dar es Salaam.
 
Logo ya FIESTA 2010
Jukwaa likiwa limefurika mashabiki saa nane mchana kabla ya shoo kuanza
Tangazo la Vitamalt Plus, moja ya matangazo ya kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) wadhamini wa Fiesta, likiwa katika uwanja huo wa Jamhuri.
Wadau wakiendelea kumiminika kuingia uwanjani
Wadau wakiwa katika foleni ya tiketi

Maelfu ya wadau ndani ya 'nyumba'
Mmoja wa mashabiki akiwa amembeba mtoto wake apate naye kuona uhondo uliokuwa ukiendelea
Watu mzukaaaaa
Mama huyu mwenye mtoto akiingia na mwanae kufaidi mambo
Jamaa akajifanya mjuaji akakutana na ulinzi mkali wa polisi uliokuwepo 
"Kaka hii kamera kiboko" inaelekea ndivyo alivyokuwa anasema huyu jamaa wa Clouds tv alipoijaribu kamera ya Michuzi Jr (kushoto)
Mzee wa Mabagala (mwenye tai) akiwa na baadhi ya wasanii kabla ya kuanza ' ukamuaji'
MMOJA wa mashabiki waliohudhuria onyesho la Fiesta lililofanyika katika Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro, Cuthbert Aloyce, akionyesha umahiri wake wa kucheza 'sebene' aliposhindanishwa na wenzake wanne kusakata muziki jukwaani. Aloyce aliwashinda wenzake na kupata zawadi ya sh. 20,000 na kugharamiwa kila kitu na waandaaji kwenda katika Fiesta itakayofanyika dar es Salaam. Maonyesho ya Fiesta yanaratibiwa na Prime Times Promotions kwa udhamini wa bia aya Serengeti inatotengenezwa na kampuni ya bia hiyo hapa nchini (SBL).
Vijana wa Offside trick wakikamaua na 'pole samaki'
Wakamuaji kutoka Tip Top Connection wakiwajibika
Ma-repoter nao muhimu, walikuwepo tele ndani ya nyumba!  

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages