MAMLAKA ya Maji Safi na Maji Taka mkoa wa Dar es Salaam (DAWASCO), imesema asiliam 53 ya maji yanayozalishwa Dar es Salaam hayawafiki wananchi.
Akizungumza na waandishi wa habari jana Mkurugenzi wa Dawasco Jackison Midala alisema tatizo hilo linachangiwa na wananchi wengi kuharibu miundombinu ya maji na kulisababishia hasara kubwa mamlaka hiyo.Alisema maerneo ya Tabata na Kimara yanaongozwa kwa wizi wa miundombinu ya maji na hivi sasa wamejipanga kukabiliana na tatizo hilo. Midala alisema mamlaka yake inatarajia kuwashirikisha wenyeviti wa serikali za mitaa na vikundi vya ulinzi shirikishi kukabiliana na tatizo hilo.
“Tatizo la wizi wa miundombinu ya maji Dar es Salaam bado ni kubwa, tumeamua kuwashirikisha wenyeviti wa serikali za mitaa ili kudhibiti tatizo hilo,” alisema.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi huyo zaidi ya wateja 21,000, wanatarajiwa kufungiwa mita za maji mwishoni mwa mwaka huu.
Alisema mita 10 zilizofungwa kwa ajili ya majaribio kwenye maeneo tofauti mjini Dar es Salaam zimebainika hazina matatizo. Akizungumzia mita za luku alisema wataanza kuziuza mwishoni mwa mwaka huu na mita moja itauzwa kwa sh. 2,60,000.
Mtendaji Mkuu wa Shirika la Majisafi na Majitaka Dar es Salaam, (DAWASCO), Jackson Midala, akizungumza na waandishi wa habari, katika ofisi za shirika hilo, Dar es Salaam, jana. Kulia ni Ofisa Habari wa DAWASCO, Mary Lyimo
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269