• MAUAJI YA ALBINO YATAJWA
NA MWANDISHI MAALUM,NEW YORK
Nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa zilizotia sahihi na kuridhia Makubaliano ya Haki za watu wenye ulemavu, zimemaliza mkutano wao wa siku tatu, huku wito ukitolewa kwa zile nchi ambazo bazo hajiyaridhia au kutia sahihi makubaliano hayo kufanya hivyo haraka.
Balozi wa Mexico katika Umoja wa mataifa, Bw. Claude Heller ambaye alikuwa rais wa mkutano huo ambazo ni watatu tangu kupitishwa kwa makubaliano hayo mwaka 2008, akihitimisha mkutano huo anasema hadi wakati mkutano huo unamalizika ni nchi 146 kati ya 192 ambazo zimetia sahihi wakati nchi 90 zimeuridhia.
Akasema ingawa idadi hiyo inatia moyo, lakini ili makubaliano hayo yaweze kuwa na nguvu kubwa na yakatetekelezwa kwa ukamilifu,ni vema nchi zote 192 tikatia sahihi na kuridhia makubaliano hayo.Idadi
Mamia ya wajumbe kutoka serikalini, vyama visivyo ya kiserikali huku wengi wao wakiwa na walemavu wa ina mbalimbali,walishirikiana na wataalamu kutoka sekretarieti ya Umoja wa Mataifa na mashirika yake , kujadili, kutafakaRi na kupanga mbinu na mikakati ya namna bora zaidi inayoweza kufanikisha utekelezaji wa makubaliano hayo.
Mkutano huo pamoja na masuala mengine ulijadili kuhusu Mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi (albino), elimu mjumuisho , ajira , afya na mazingira duni na hatarishi wanayoishi watu wenye ulemavu.
Takwimu zinaonyesha kuwa dunia ina watu takriban milioni 650 wenye ulemavu wa aina mbalimbali, huku idadi ikiendelea kuongezeka kutoka na majanga ya asili kama vile mafuriko, matetemeko vita na machafuko.
Akito taarifa ya kikao kilichokuwa kikijadili hali ya watu wenye ulemavu katika mazingira hatari na wakati wa dharua, Bi Diane Richeler amewaeleza washiriki kwamba katika kikao hicho kimebaini kuwa watu wenye ulemavu wamekuwa wa mwisho au hawakumbukwi kabisa inatopotea dharura kama vile matetemeko, mafuriko au majanga ya vita na migogoro.
Akasema kuwa hali inatakiwa kubadilika sasa na hasa ikizingatiwa kwamba kumekuwapo na ongezeko la majanga asilia, kama yale yaliyotokea Pakstani, Haiti na China.Hali inayozilazimu serikali kuweka mipango rasmi inayoainisha namna ya kuwahudumia watu wenye ulemavu inapotokea dharua.
Anaongeza kwa kusema katika maeneo mengine na bila ya kutaja nchi, dunia imendelea kusikia taarifa za mauaji ya albino hasa Afrika, yakiwamo mauaji ya watu wanaosingiziwa kujihusisha na vitendo ya uchawi kwa vile tu wanamatatizo ya ulemavu wa aina fulani.
Akasisitiza kuwa makundi hayo ya walemavu yanahitaji pia uangalizi na ulinzi kutoka serikali kwa kile alichosema ni makundi ambayo hayawezi kujitetea yenyewe.
Ujumbe wa Tanzania katika mkutano huo uliongozwa na Bw. Msham Abdalla Khamis,Katibu Mkuu Afisi ya Waziri Kiongozi serikali ya Mapinduzi Zanzibar, aliyefuatana na Bi Abeida Rashid Abdalla, Mkurugenzi wa Idara ya Walemavu, Afisi ya Waziri Kiongozi.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi, mara baada ya kumalizika kwa mkutano huo, Katibu Mkuu ameelezea kusikitishwa kwake na ushiriki mdogo wa Tanzania katika mkutano huo ambazo ameueleza kuwa unaumuhimu wa aina yake hasa pale ambapo serikali ya Jamhuri ya Muungano imeonyesha utashi mkubwa wa kisiasa wa siyo tu kuyaridhia makubaliano hayo bali hata kuanza kutekeleza baadhi ya vipengele.
Akasema pande zote mbili za muungano zimejitahidi katika kuboresha baadhi ya sheria na kutunga sera zinazolenga kuboresha maisha ya watu wenyeu lemavu, ingawa anakiri kubwa bado kuna safari ndefu. Na kwamba hakuna mahali pengine pa kuyaelezea mazuri yaliyokwisha kufanyika zaidi ya mikutano hiyo ya kimataifa.
“ Nimesikitika kidogo kwa mahudhurio yetu duni, si kwa upande wa serikali tu hata NGO hakuna NGO hata moja kutoka Tanzania, wenzetu wamekuja kwa umoja wao. Hii ni mikutano ya kikazi, tunajifunza mengi kwa kuhudhuria, tunapata fursa ya kujua wenzetu wamefanya nini au wanafanya nini, lakini ni mahali pia ambapo hata sisi tunapata fursa ya kueleza kile ambacho tumekwisha kufanya, lakini huwezi kufanya hivyo kama huhudhurii au unahudhuria nusunusu tu” anasema Katibu Mkuu
Akasema swala la kujiandaa ni muhimu sana, na ingawa asingependa kumyoshea kidole mtu yeyote, anahimiza maandalizi ya mapema ili wahusika waweze kuhudhuria mikutano hiyo badala ya kuhudhuria kwa kubahatisha bahatisha.
Katibu Mkuu Msham Khamisi anaelezea zaidi kwa kusema kuwa kwa vile mikutaho kama hii hujulikana mapema na kama ule utakaofanyika mwakani mwezi wa tisa basi maandalizi yaanze mapema. Ili angalau huo mkutano wa mwakani uwakilishi wa Tanzania uwe mzuri na wenye tija.
MJUMBE AMBAYE NI MLEMAVU WA KUTOKUWA NA MIKONO AKIANDIKA KWENYE KOMPYUTA YAKE KWA KUTUMIA MIGUU, MAJADILIANO YALIYOKUWA YAKIEDELEA KUHUSU HAKI ZA WATU WENYE ULEMAVU WAKATI WA MKUTANO WATATU WA UMOJA WA MATAIFA WA NCHI WANACHAMA ZILIZOWEKA SAHIHI NA KURIDHIA MAKUBALIANO YA HAKI ZA WATU WENYE ULEMAVU.
KATIBU MKUU, . MSHAM ADBALLA KHAMIS AFISI YA WAZIRI KIONGOZI SERIKALI YA MAPINDUZI ZANZIBAR AKIONGOZA UJUMBE WA TANZANIA KATIKA MKUTANO WA UMOJA WA MATAIFA WA MAKUBALIANO KUHUSU HAKI ZA WAT WENYE ULEMAVU. NYUMA YAKE NI BI ABEIDA RASHIDI ABDALLA, MKURUGENZI WA IDARA YA WALEMAVU AFISI YA WAZIRI KIONGZI AMBAYE NI NI MLEMAVU WA MIGUU AKIFUTATILI MAJADILIANO.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269