Breaking News

Your Ad Spot

Oct 31, 2010

UCHAGUZI MKUU TANZANIA WAFANYIKA LEO

Rais Jakaya Kikwete leo ameongoza Watanzania kuoiga kura katika uchaguzi mkuu wa Rais, Wabunge na Maadiwani na Rais Abeid Amani Karume akiongoza kwa upande wa Zanzibar. Pichani rais Kikwete akipiga kura yake kijiji cha Msoga, mkoa wa Pwani. 
Karume akipiga kura Kituo cha Kiembesamaki, ZanziRais bar. 
Dk. Gharib Bilal akipiga naye pia kura yake katika kituo hicho. Bilal ni mgombea mwenza kwa tiketi ya CCM 
Mgombea Urais wa Zanzibar, Seif Sharif Hamad, yeye alipiga kura yake katika kituo cha Skuli ya Mtopepo Wilaya ya Mjini 
Wananchi wakiwa wamefurika katika kituo cha kupiga kura cha Shule ya Mtoni, wilaya ya Mjini. 
Ilikuwa asiye na mwana abebe jiwe, kama  Zainabu Ngwadani mkazi wa Mtoni Kidalu, wilaya ya Magharibi, akipiga kura huku akiwa na mtoto wake mwenye umri wa miezi mitano, katika kituo cha shule ya Mtoni
Amina Mohammed (80), liha ya uzee alio nao, akamuomba msaada kijana kumpeleka kituo cha kupiga kura cha Mwanakwerekwe, akapiga. 

Kisha Bibi huyu akabebwa kuingizwa katika gari kurudi nyumbani baada ya kupiga kura yake. 
Polisi nao wakawa na kazi ya ziada ambapo pamoja na ulizni lakini pia wakawa na jukumu la kusaidia wazee na wengine waliohitaji msaada. Pichani, polisi akimsaidia Bi , Swaumu Mbaraka Fumu ili aende kupiga kura yake katika kituo cha Ban Bella, Zanzibar.
Mvua nayo ilikuwa na kasherehe ya aina yake baada ya kudamka ikinyesha asubuhi na mapema, katika muda ule ambao wapigaakura wengi walitaraajiwa kujitokeza vituoni. pichani watu waliofika kituo cha Kimbe Sakmaki kupiga kura, wakijificha mvua hiyo. 
Musimu Hassani Ali akipiga kura yake mapemaaa kutuo cha Ben Bella

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages