SERIKALII wilayani Kwimba imesema kwamba, itawakamata na kuwafikisha kwenye mkono wa sheria wanasiasa watakaotumia majukwa kuitukana, kufanya uchochezi na kuhatarisha amani.
Akihutubia maelfu ya wananchi waliohudhuria mkutano wa kupinga maandamano ya uchochezi, hivi karibuni mjini Ngudu, Mkuu wa wilaya ya Kwimba Christopher Kangoye alisema wanasiasa ‘uchwara’ wasiifanye Kwimba uwanja wa kupangia vurugu na uchochezi. Kangoye ambaye ni Mtemi wa jeshi la jadi la wilaya hiyo (Sungusungu) alisema hayo baada ya kupokea heshima na salamu za askari zaidi ya 2,000 wa jeshi hilo , waliodai kwamba wamechoshwa maandamaono na mikutano ya uchochezi ya wanasiasa.
“Tutawakamata wanasiasa wanaodai wanakuja kufanya mikutano kwa nia nzuri kisha wanatumia fursa hiyo kufanya uchochezi, kumtukana Rais na Serikali, Kwimba siyo uwanja wa kupangia uchochezi,” alisema Mkuu huyo wa wilaya.
Alieleza kwamba nchi yetu imejengwa kwa misingi imara ya demokrasia, amani, mshikamano na umoja wa kitaifa ambao unapaswa kulindwa kwa nguvu yote na kila mmoja, hivyo kuruhusu kundi la watu waivuruge ni kuuza amani ya watanzania.
Alisema maelfu ya sungusungu hao, wananchi, viongozi wa vyama vya siasa, Vitongoji, Vijiji, Kata na wilaya waliohudhuria kwenye mkutano huo wa kupinga siasa za uchochezi zinazoweza kuvunja amani ya nchi, ni ishara kwamba wana Kwimba wanataka amani siyo mambo ya Tunisa au Libya .
Sungusungu hao wakiongozwa na Mteni wa Tarafa ya Ibindo Shimbi Mogani, wakiimba nyimbo za kusisitiza amani kwa lugha ya kisukuma, walisema uchaguzi umekwisha wana Kwimba wanachapa kazi na kusomesha watoto kuondoa umaskini na ujinga, waachiwe amani waliyozoea.
Waliimba “Obebe Slaa nelechama lyako mle bayojase.” Yaani wewe Dk Slaa na chama chako ni wachonganishi na kuwaasa wananchi wasiwape nafasi ya kuchochea vurugu na pia kumtaka Mtemi wao (Kangoye) achukue hatua kama serikali wilayani mwake wanapotokea wachochezi.
Awali mkutanao huo ulitanguliwa na maombi ya sala kuiombea nchi iwe na amani na kuepuka vurugu kama za Misri, Tunisia na Libta, kabla ya jeshi hilo kutoa heshina na nasaha hizo.
Waliotoa maombi hayo ni Sheikh Mkuu wa wilaya ya Kwimba Sad Seif (BAKWATA) na Mwenyekiti wa Umoja wa Makanisa wilayani humo, Mchungaji Samuel Makima (AICT Kwimba) ambao walisema kuwa
uchaguzi ulisha isha viongozi wakapatikana hivyo wajibu wa kila moja ni kutii mamlaka ya serikali.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269