NA FRANCIS GODWIN, IRINGA
Chama cha mapinduzi (CCM) mkoa wa Iringa kimeanza kufuatilia utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi katika Halmashauri ya Manispa ya Iringa kwa kutembelea miradi mbali mbali ya kimaendeleo.
Katibu wa CCM ,mkoa wa Iringa Mary Tesha amesema kuwa lengo la ziara hiyo ni kuona jinsi ambavyo ilani ya CCM ilivyoanzwa kutekelezwa mara baada ya uchaguzi mkuu uliofanyika mwaka jana .
Amesemea kuwa katika ziara hiyo CCM imefurahishwa na utekelezaji wa Ilani yake katika Manispaa ya Iringa na kutaja baadhi ya maeneo ambayo yamefanywa vizuri kuwa ni pamoja na miradi ya ujenzi wa sjhule za sekondari,vituo vya afya na miradi mingine ya kimaendeleo.
Katika ziara hiyo iliyoanza Manispaa ya Iringa CCM mkoa pamoja na kamati ya utekelezaji ya wilaya ya Iringa mjini ikiongozwa na katibu wake Charley Charlesy kwa upande wa Manispaa ya Iringa imetembelea shule ya sekondari ya mazoezi Kleruu, kituo cha afya Ngome , shule ya sekondari Kihesa ,Mtwivila na kufanya mkutano na wananchi wa kijiji cha Nduli.
Pamoja na kupongeza jitihada mbali mbali zinazofanywa na uongozi wa shule hiyo na wananchi wa kata ya Gangilonga katika kuendeleza shule hiyo bado katibu wa CCM mkoa wa Iringa Mary Tesha aliutaka uongozi wa shule ya sekondari Mazoezi Kleruu kueleza sababu ya shule yake kukosa walimu .
Alisema kuwa kimsingi shule hiyo ni sehemu ya nyenzo za kufundishia walimu katika chuo cha ualimu Kleruu na ndio sababu ya serikali kujenga shule hiyo ndani ya majengo ya chuo cha ualimu Kleruu hivyo uongozi wa shule hiyo kulia juu ya tatizo la walimu ni jambo la kushangaza .
“Tumefurahishwa sana na jitihada mbali mbali zinazofanywa na kamati ya ujenzi na wananchi wa kata hii ya Gangilonga pamoja na Manispaa ya Iringa katika kuboresha elimu Manispaa ya Iringa …ila kwa hili la kukosa walimu wa kutosha hapa shule ya sekondari Kleruu tunaomba maelezo ya kutosha” alisema katibu huyo.
Kwani alisema kuwa lengo la ziara ya CCM katika Halmashauri ya Manispaa ya Iringa ni kutaka kuona jinsi ambavyo ilani ya CCM ilivyoanzwa kutekelezwa baada ya uchaguzi mkuu uliofanyika mwaka 2010 ili kuona changamoto mbali mbali zinazokwamisha utekelezaji wa Ilani hiyo na mafanikio ya utekelezaji wa kipindi kifupi ambacho Rais Jakaya Kikwete ameingia madarakani.
Kwa upande wake mstahiki Meya wa Manispaa ya Iringa Amani Mwamwindi alisema kuwa Halmashauri hiyo ina jukumu kubwa ya kusimamia kwa umakini utekelezaji wa Ilani ya CCM na kuwa siku ya kwanza kabisa ya kuanza kwa baraza jipaya la madiwani mkurugenzi wa Halmashauri hiyo alikabidhiwa Ilani ya CCM kama kitendea kazi namba moja katika kutekeleza ahadi za serikali iliyopo madarakani.
Kwa upande wake mkuu wa shule ya Mazoezi Kleruu Yoram Mponzi alisema kuwa shule hiyo ina jumla ya walimu 17 japo awali kabla ya walimu 12 kwenda masomoni ilikuwa na walimu 28.
Hata hivyo alisema kuwa sababu kubwa iliyopelekea shule hiyo kuwa na upungufu wa walimu ni kutokana na utaratibu mpya wa wizara ya elimu ambapo ulisitisha utaratibu wa shule hiyo kuchagua walimu wanaohitimu katika chuo hicho kufundisha shule hiyo kabla ya kupangiwa walimu na katibu mkuu wa wizara ya elimu.
Hata hivyo alisema kuwa sababu kubwa iliyopelekea shule hiyo kuwa na upungufu wa walimu ni kutokana na utaratibu mpya wa wizara ya elimu ambapo ulisitisha utaratibu wa shule hiyo kuchagua walimu wanaohitimu katika chuo hicho kufundisha shule hiyo kabla ya kupangiwa walimu na katibu mkuu wa wizara ya elimu.
Pia alisema shule hiyo iliyoanzishwa mwaka 2002 ina jumla ya wanafunzi 842 wakiwemo wasichana 412 na wavulana 430 na ina kidato cha 1-IV.
Vyumba vya madarasa vilivyopo ni 16 maktaba ipo japo haijakamilika ,maabara vyumba 2 havijakamilika na chumba kimoja kiko kwenye hatua ya umaliziaji ,matundu ya vyoo vya wanafunzi 16.
Huku matundu ya walimu ya shule hayopo kabisa zaidi ya kutumia yale ya chuo cha ualimu pekee.
Katika hatua nyingine wafanyakazi wa zahanati ya Ngome wamelalamikiwa kwa kutoa majibu mabaya kwa wagonjwa pindi wafikapo kupata huduma za afya
Malalamiko hayo yametolewa mbele ya katibu mkuu wa chama cha mapinduzi mkoani Iringa Mary Tesha wakati alipofanya ziara yake katka zahanati hiyo ikiwa ni mikakati ya kutimiza ilani ya chama hicho
Mwenyekiti wa matta wa Ngome Mario Mponzi amesema kuwa kumekuwepo na tabia ya wauguzi wa zahanati hiyo kutoa majibu yasiyofaa kwa wagonjwa hali inayopelekea wananchi katika eneo hlio kukikimbilia katika hospitali ya mkoa kufuata huduma wanazo hitaji
Your Ad Spot
Apr 1, 2011
Home
Unlabelled
CCM Iringa yaanza kuzibana Halmashauri juu ya utekelezaji wa Ilani
CCM Iringa yaanza kuzibana Halmashauri juu ya utekelezaji wa Ilani
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Top Ad
Your Ad Spot
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269