Kitendawili cha timu ipi itatwaa ubingwa ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom, kinatatuliwa leo, baada ya mechi nne za kufunga ligi hiyo zitakaporindima jioni hii kwenye viwanja tofauti. Kutokana na msimamo ulivyo hadi kufikia leo, inadhaniwa na wadau wengi wa soka kwamba huenda upangaji matokeo ukajitokeza katika mechi hizo za lala salama hasa kwa upande wa Yanga na Simba. Hali ya mambo inaonyesha kwamba Yanga wanaweza kupewa nafasi ya kushinda mabao mengi wanayohitaji, watakapomenyana na wadogo zao, Toto Africa katika mechi yao inayopigwa kwenye Uwanja wa CCM Kirumba.
Wakati kwa Yanga hali ikidhaniwa hivyo Simba nayo inaonekana huenda ikabebwa na rafiki zao Maji Maji ya Songea, katika mechi yao itakayopigwa kwenye Uwanja wa Uhuru aka Shamba la Bibi mjini Dar es Salaam.
Matumaini ambayo yanadhaniwa pia kuwa yanaweza kuipa Yanga au Simba ni pale moja ya timu kati ya Maji Maji au Toto Africa, ikiamua kukacha kuingia uwanjani na hivyo ikawa kwa mfano Simba imejipatia mabao matatu na poiti zake tatu hali ambayo itakuwa maafa kwa Simba kama mjini Mwanza Yanga itakuwa imepata mabao ya kutosha kwa Toto Africa.
Mechi nyingine za kufunga dimba ni Africa Lyon na Mtibwa kwenye Uwaja wa Manungu uliopo nje ya mji wa Manungu, Kagera Sugar ikikwaana na Arusha FC ndani ya Kaitaba mjini Bukoba na Ruvu Shooting na Azam uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.
Your Ad Spot
Apr 10, 2011
Home
Unlabelled
UBINGWA LIGI KUU YA VODACOM: NI SIMBA JUU YA MABEGA YA MAJIMAJI DAR AU YANGA JUU YA MABEGA YA TOTO AFRIKA MWANZA
UBINGWA LIGI KUU YA VODACOM: NI SIMBA JUU YA MABEGA YA MAJIMAJI DAR AU YANGA JUU YA MABEGA YA TOTO AFRIKA MWANZA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Top Ad
Your Ad Spot
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269