CHAMA CHA MAPINDUZI
OFISI NDOGO YA MAKAO MAKUU S.L.P. 9151 DAR ES SALAAM F2180108
Barua zote zipelekwe kwa Katibu Mkuu Fax: 255-022-2185245; 022-2184580
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya Taifa itafanya ziara ya siku nne (4) Mkoani Rukwa kuanzia tarehe 31 Mei, 2011. Pamoja na mambo mengine ziara hiyo itakuwa na dhumuni la kukutana na wanaCCM na Wapenzi wa CCM na kufikisha maamuzi ya Halmashauri Kuu ya Taifa iliyofanyika tarehe 10-11 Aprili, 2011.
Katika ziara hiyo, ujumbe huo wa Sekretarieti utaongozwa na Ndugu Nape M. Nnauye, Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa – Itikadi na Uenezi. Kutokana na ziara hiyo, wanaCCM, Wakereketwa, wapenzi wa CCM na wananchi kwa ujumla wao wanaombwa kuhudhuria mikutano ya hadhara inayotarajiwa kufanywa katika maeneo mbalimbali kama ratiba inavyoonyesha.
Ratiba ya ziara hiyo ni kama ifuatavyo hapa chini:-
TAREHE | MUDA | SHUGHULI | MAHALI | MHUSIKA | |
31/5/2011 | 3.30-400 | Mapokezi | Mji Mdogo wa Laela (Barabara Kuu) | Viongozi wa CCM Mkoa | |
4.00-6.00 | Mkutano wa Hadhara | LAELA | Katibu wa Wilaya | ||
6.00-7.30 | Kuelekea Sumbawanga Mjini | Katibu wa Mkoa | |||
8.00-12.00 | Mkutano wa Hadhara | Uwanja wa Mandela | Katibu wa Wilaya | ||
1/6/2011 | 4.00-6.00 | Mkutano wa Hadhara | Namanyere (Wilaya ya Nkazi) | Katibu wa Wilaya | |
9.00-11.00 | Mkutano wa Hadhara | Kabwe | Katibu wa Wilaya | ||
11.00-12.30 | KUELEKEA MAJIMOTO (KULALA) | ||||
2/6/2011 | 4.00-6.00 | Mkutano wa Hadhara | Maji Moto | Katibu wa Wilaya | |
8.00-11.00 | Mkutano wa Hadhara | Usevya | Katibu wa Wilaya | ||
KULALA MPANDA | |||||
3/6/2011 | 4.00-6.00 | Mkutano wa Hadhara | Kakese | Katibu wa Wilaya | |
9.00-12.00 | Mkutano wa Hadhara | Mpanda Mjini | Katibu wa Wilaya | ||
Imetolewa na:
Nape M. Nnauye,
KATIBU WA HALMASHAURI KUU YA TAIFA
ITIKADI NA UENEZI
29/5/2011
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269