Meneja Mawasiliano wa Vodacom Tanzania Salum Mwalim akiwaonyesha moja ya jarida(Voda World) linalotolewa na Kampuni hiyo baadhi ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Tumaini cha Iringa wanaosomea kozi ya mambo ya habari walipotembelea makao makuu ya kampuni hiyo kujifunza mambo mbalimbali yanayofanywa katika kitengo cha Mawasiliano na masoko ya kampuni hiyo hivi karibuni.
Mmoja wa wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Tumaini cha Iringa anaesomea kozi ya mambo ya habari akiuliza swali walipotembelea makao makuu ya kampuni ya Vodacom Tanzania kwa ajili ya kujifunza mambo mbalimbali yanayofanywa na Kampuni hiyo katika kitengo cha Mawasiliano na masoko. Baadhi ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Tumaini cha Iringa wanaosomea kozi ya mambo ya habari wakisoma jarida(Voda World) linalotolewa na Vodacom Tanzania bure mara walipotembelea makao makuu ya kampuni ya hiyo kwa ajili ya kujifunza mambo mbalimbali yanayofanywa na Kampuni hiyo katika kitengo cha Mawasiliano na masoko. Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano wa Vodacom Tanzania Nector Foya wa tatu kutoka kulia akiwaonyesha baadhi ya wanafunzi wa Chuo kikuu cha Tumaini cha Iringa namna ripoti zinavyoandaliwa na kitengo cha Mawasilino cha Vodacom Tanzania mara walipotembelea makao makuu ya kampuni hiyo kwa ajili ya kujifunza mambo mbalimbali yanayofanywa na Kampuni hiyo katika kitengo cha Mawasiliano na masoko.
Ni vyema kutembelea vitu kama hivyo, unaifunza kivitendo au sio?
ReplyDelete