NA MWANDISHI WETU, MOROGORO
KATIBU wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye (Pichani) , amesema bajeti ya mwaka 2011/2012 imelenga kutatua kero zilizojitokeza kwenye elimu ya juu .
Nape alisema hayo jana mjini Morogoro wakati akizungumza na wanafunzi wa elimu ya juu kwenye sherehe ya kuwaaga makada wa CCM waliokuwa wakisoma Chuo Kikuu cha Kiisilamu mjini hapa.
Akitolea mfano uamuzi wa serikali kutoza kodi ya kukuza ujuzi, ambayo katika hiyo ya 2011/2012 mgawanyo wake umelenga kupeleka asilimia 4 kati ya 6 ya kodi hiyo kwenye Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu hivyo kuongeza uwezo wa bodi hiyo kuhudumia wanafunzi.
“mwaka jana kodi hii ilikusanya karibu sh. bilioni 200, na huwa inaongezeka kadri uchumi unavyokua, mategemeo kwa mwaka huu wa fedha , fedha hii itaongezeka hivyo kutenga aslilimia hiyo itasaidia sana kwenye kutatua tatizo la mikopo kwa elimu ya juu”Alisema Nape
Aliwataka wanafunzi kuwapuuza wanaopita na kusema hakuna kilichofanywa na serikali huku wakijua wazi kuwa kila mwaka hatua kubwa inapigwa katika kushughulikia kero mbalimbali za wananchi ikiwemo sekta ya elimu.
“kumekuwa na maneno mengi juu utaratibu wa kutoa mikopo na uendeshaji wa bodi yake, kwa kulitambua hili Rais Jakaya Kikwete ameunda tume ya kuangalia namna bora ya kushughulika na hili la bodi, tume ikikamilisha, na hili ongezeko la fedha bila shaka changamoto nyingi zitapungua” alisema Nape.
Katika sherehe hiyo Nape alikabidhi vyeti kwa makada 65 wa CCM waliohitimu chuo hicho na kupewa taarifa ya chama ya tawi la CCM la wasomi hao.
Mjini Morogoro, Nape na msafara wake walipokewa na viongozi wa CCM mkoa huo wakiongozwa na Mwenyekiti wa CCM mkoa, Petro Kingu.
Your Ad Spot
Jun 12, 2011
Home
Unlabelled
BAJETI IMELENGA KUTATUA KERO ZA ELIMU YA JUU:NAPE
BAJETI IMELENGA KUTATUA KERO ZA ELIMU YA JUU:NAPE
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Top Ad
Your Ad Spot
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269