Breaking News

Your Ad Spot

Jun 18, 2011

FAMILIA YA MZEE KAWAWA YAINGIA KATIKA MGOGORO WA KIFAMILIA

Na Mwandishi wetu Dodoma.
IKIWA ni takriban mwaka mmoja sasa tangu kufariki,  Simba wa Vita, Mzee Rashid Kawawa (pichani),kufariki dunia familia yake imeingia katika mgogoro baada ya mjane wake  kudaiwa kuamua kupangisha moja ya nyumba ya marehemu bila ridhaa ya familia.
Mmoja wa watoto wa hayati Kawawa Zainabu Kawawa alisema tkatika hali  ambayo hawakutarajia mama yao huyo ameamua kuwatimua katika nyumba hiyo ili apangishe.
Zainabu ambaye alikuwa akizungumza na waandishi wa habari, mjini hapa, alisema mama yao huyo ameamua kuipangisha nyumba hiyo iliyoko katika eneo la Kilimani bila kuwahusisha wanafamilia wakiwemo watoto hao wa  marehemu.
Alisema mama huyo anadai kuwa nyumba hiyo amerithishwa na marehemu mume wake kabla umauti hauja mfika.

"Sisi kama watoto hatuna taarifa yeyote kama baba alimpa nyumba hii mama yetu" alisema Zainabu.
Alisema wao kama watoto hawana tatizo na nyumba hiyo kwani wanazo nyumba zao lakini wanachokataa ni kupangishwa kwa nyumba hiyo ambayo kwa hapa dodoma ni kama kumbukumbu yam zee kawawa.

"Sisi tunachosema hii ni kumbukumbu ya Baba yetu na sisi tunapokuja Dodoma tunafikia hapa na hata watu mbalimbali wanajua hivyo iweje leo ipangishwe" alihoji Zainabu.

Alisema kuwa mama yao huyo amemua kuchukua mkopo toka Benki ya CRDB zaidi ya sh.milioni 74 kwa udhamini wa nyumba hiyo na hadi sasa deni  la mkopo huo limeshafikia hadi sh milioni 102 kutokana na kutolipwa jambo ambalo linahatarisha nyumba hiyo kupigwa mnada, vinginevyo familia inapaswa kulipa sh.a sh milioni nane kila mwezi benki.

"sisi tumekubali mama kumlipia hilo deni lakini bado hataki anachotaka kuipangisha nyumba sasa ni mpangaji gani anaweza kulipa sh milioni nane kwa mwezi nyumba hii" alihoji Zainabu.

Kuhusu tuhuma hizo, mjane huyo wa Mzee Kawawa, Asina Kawawa amesema nyumba hiyo ni mali yake na ana uwezo wa kufanya chochote.

Alisema nyumba hiyo aliachiwa na Mumewe baada ya kuinunua toka serikalini mwaka 2007.
" Mimi namshangaa huyu mtoto mimi nyumba hii amenirithisha marehemu mume wangu sasa yeye anachokataa ni nini mimi kuipangisha si yangu" alisema mama huyo.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages