.Asema sheria haifutwi barabarani
Nape Nnauye |
KATIBU wa Itikaddi na Uendezi CCM, Nape Nnauye amesema madai ya viongozi wa Chadema kutaka posho za watumishi wa serika na wabunge zifutwe ni unafiki na ajenda ya kusaka umaarufu wa kisiasa lakini siyo hoja inayotoka katika dhati ya mioyo yao.
Akizungumza kwaa njia ya simu, leo, Nape alisema, viongozi hao wa Chadema wangekuwa na dhamira za dhati kutaka posho hizo zifutwe wangefuata taratibu zinazojulikana ambazo ni za uhakika badala ya kumwandikia spika barua na kuzungumzia swala hilo barabarani.
Nape alisema, kwa kuwa utaratibu huo wa posho uliwekwa kisheria baada ya kupitishwa na bunge, viongozi hao wa Chadema kama wangekuwa wa
kweli kutaka posho hizo zifutwe wangepeleka hoja hiyo bungeni kwa kuwa inazungumzika.
"Badala ya kuzungumzia barabarani kuhusu jambo hili ambalo linazungumzika, kama kweli wana nia hiyo na si vinginevyo wapelekehoja binafsi bungeni ambako ndiko sheria hutungwa" alisema Nape.
"Kimsingi sina tatizo na hoja kwasababu wanahaki kuitoa, lakini nina mashaka na dhamira yao hasa njia wanayotumia kuijadili hoja hii" alisema.
Alionyesha kumshangaa, Mwenyekiti wa Chadema , Freean Mbowe kuweweseka na utaratibu huo wa posho ili hali ulipitishwa kisheria kwa kujadiliwa na wabunge katika bunge ambalo na wabunge hao wa upinzani walikuwemo.
Kuhusu hoja ya Mbowe kwamba posho za watumishi wa serikali zingefutwa zingeweza kupatikana sh. bilioni 900 kwa mwaka, Nape alisema, watumishi wa serikali kama polisi, walimu, na wataalam mbalimbali wanapoajiriwa kwa ajira mpya hupewa nauli na posho za kujikimu
kuwawezesha kufika vituo vya kazi.
"je, ikiwa utaratibu huo wa posho utafutwa kabisa kama wanavyodai, wafanyakazi hawa watakuwa wanafika vipi kwenye vituo vyao vya kazi ?" alihoji Nape.
Nape alisema, suala la msingi ni kwamba serikali ifute posho zisizo za lazima kwa kuwa haiwezekani kufuta hata zile za muhimu, na kutaka suala hilo lijadiliwe kwa kuzingatia uhalisia wake siyo kwa mlengo wa kisiasa.
"Hata hivyo waziri wa fedha ameshasema serikali itafuta posho zisizokuwa za lazima, lakini huwezi kufuta posho zote" alisisitiza Nape na kuwataka wananchi kuwa makini na ghiliba za kisiasa zenye lengo la kutafuta umaarufu kisiasa badala yake wapime kila hoja.
"Na kwa Chadema hii ni kama kawaida yao, wanapoona hawana hoja za msingi, hukimbilia kuzusha mambo ambayo hata wao huwa hawayaamini, mfano ni wakati Katibu Mkuu wa Chama hicho, Dk. Wilbrod Slaa alipokuwa mbunge alizusha hoja kwamba anaumizwa na mshahara wa wabunge wa sh. milioni 6, kwamba ni mkubwa mno kulingana na hali za vipato vya
Watanzania walio wengi.
Baada ya kutamba na hoja hiyo kiasi cha baadhi ya wananchi kudhani anakerwa na hali hiyo, sasa yeye mwenyewe amedai na kupata malipo ya Sh. milioni 7 kila mwezi kutoka Chadema huku wafanyakazi wengine wa chama hicho wakipata malipo yasiyofikia hata robo ya kiasi hicho.
" Mheshimiwa Mbowe akatoka hadharani kumtetea Dr. Slaa kuwa eti malipo ya 7.5 milioni kwa mwezi ni posho tu isiyostahili kulipiwa kodi,leo wanadai kuona uchungu kwa posho za wengine!! Narudia sina tatizo na hoja ila ninatatizo na dhamira yao" alimalizia Nape
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269