Na Mwandishi Wetu
KAMPUNI mpya ya kuibuka vipaji vya wasanii, kuendeleza na kusambaza kazi zao, Pappa-Zi, imetangaza mikakati mpya ya kutimiza malengo yake kuanzia sasa, imefahamika juzi jijini Dar es Salaam. Kwa Mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari iliyosambazwa jana jijini Dar es Salaam, Meneja Masoko wa kampuni hiyo, Issa Kipemba, amesema kwamba taasisi hiyo ni mpya ambayo makao yake makuu yako Mikocheni “B” kwa Warioba, jijini Dar es Salaam.
Alisema kwamba kampuni hiyo imepanua kufanya makubwa ikianzia kufanya kongamano na wadau wa filamu litakalofanyika Juni 21, mwaka huu (Jumanne) kwenye Ukumbi wa Villa Park Resort.
Katika kongamano hilo, Rais wa Shirikisho la filamu Tanzania, anatarajiwa kuwa mmoja wa watoa mada za kuhamasisha wasanii waliokata tamaa kurejea kwenye ulingo wa kufanya kazi hiyo ya kuelimisha, kuburudisha na kufundisha kwa malengo ya kutengeneza jamii.
Alisema kwamba katika kongamano hilo wanatarajia kuibuka mawazo mapya ya kubadilisha taswira ya filamu nchini baada ya kuzoeleka hali aliyoita ni ya mazoea.
“Kila kukicha katika filamu hakuna jipya, utakuta wasanii ni wale wale, mawazo ni yaleyale, maeneo ya kuigiza ni yaleyale, na zaidi ya hapo utaona wazi kwamba tunaiga,” alisema Kipemba.
“Sasa kampuni yetu inakuja na mabadiliko tukiamini kwamba kuna wasanii zaidi ya Kipemba, kuna kusambazwa kazi zaidi ya wahindi (Watu wenye asili ya India),” alisema.
Alisema kwamba: “Huko vijijini, wilayani na mikoani kuna vipaji tofauti na sasa wanaofanya kazi. Lakini, imezoeleka kwamba unapohitaji filamu mpya, msambazaji anahoji juu ya msanii fulani kama ameshiriki, vinginevyo hanunui kwa gharama kubwa.
“Inatokea mtu unatumia Sh milioni tano kwenye kiuandaa filamu, halafu Mhindi anahoji kama fulani yumo, kama hayumo basi atasema ananunua kwa Sh milioni mbili au tatu. Hizi ni dharau,
ukiritimba ambao kampuni ya Papa-Zi imepanua kuufuta kabisa,” alisema.
Alisema kwamba kampuni yao itafanya utafiti zaidi na kwamba filamu zitakazochezwa na wasanii watakaowaibua na hata wa wenye majina kwa sasa, zitasambazwa kwa ubora wa kazi na si jina ambao wengi wamekuwa wakiiga filamu ama za kutoka India au Nigeria.
Alisema kwamba wameazimia kufanya hivyo kwa sababu ya kukataa tamaa kwa baadhi ya wasanii ambao wamekuwa “wakizibiwa” riziki na wanaopenda kujiona kwamba wao wanafamilia ya filamu.
“Ninachotaka kusema kwamba hata hao wenye majina, sasa wameanza kudharauliwa na Wahindi na wanyonyaji wengine. Kuna filamu mpya, hazina hata mwezi mmoja tangu itoke, lakini kwa sasa
inauzwa Sh 1,000 kwenye lami Buguruni au pale Ubungo,” alilalama
Your Ad Spot
Jun 19, 2011
Home
Unlabelled
KAMPUNI YA KUIBUA VIPAJI VYA WASANII, KUENDELEZA NA KUSAMBAZA KAZI ZAO 'PAPPA-Z' YATANGAZA MIKAKATI MIPYA
KAMPUNI YA KUIBUA VIPAJI VYA WASANII, KUENDELEZA NA KUSAMBAZA KAZI ZAO 'PAPPA-Z' YATANGAZA MIKAKATI MIPYA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Top Ad
Your Ad Spot
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269