Breaking News

Your Ad Spot

Jun 7, 2011

TBL YATANGAZA DAU LA SH. MILIONI KUMI MSHINDI WA KWANZA MASHINDANO YA NGOMA ZA ASILI KANDA YA ZIWA

                                                                                                NA NKOROMO DAILY BLOG
Meneja masoko wa bia ya Balimi, Fimbo Butala akizungumzia
michuani hiyo leo. Kulia ni Meneja wa bia hiyo Edith Bebwa

KAMPUNI ya bia Tanzania (TBL) kupitia bia yake ya Balimi Extra Lager, imetangaza  dau la sh. milioni moja kwa mshindi wa kwanza katika mashindano ya ngoma za asili kwa mikoa ya Kanda ya ziwa mwaka huu.


Akizungunza na waandishi wa habari, jleo mjini Dar es Salaam,  Meneja wa Balimi Extra Lager, Edith Bebwa alisema, mshindi wa pili atanyakua sh. 750,000, mshindi wa tatu sh.500,000, wa nne sh. 400,000 na mshindi wa tano hadi wa kumi  sh. 300,000 kila mmoja.


Alisema, wakati vitita hivyo ni kwa ngazi ya taifa, katika ngazi ya mikoa pia washindi watapata zawadi kwa mshindi wa kwanza kupata sh. 500,000, wapili sh. 400,000, watatu sh. 300,000, wa nne sh. 200,000 na mshindi wa tano hadi wa kumi sh. 100,000 kila mmoja.


Edith alitaja mikoa itakayoshiriki katika mashindano hayo kuwa ni Mwanza, Sinyanga, Tabora, Mara, Kagera na fainali ya michuano hiyo ambayo mwaka huu inafanyika ikiwa mara ya saba, itafanyika jijini Mwanza.


Alisema michuano hiyo itanza Juni 11 mwaka huu,  mjini Tabora  kwenye viwanja vya Chipukizi, na kuendelea, Juni 18 mkoani Mwanza kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, wakati mkoani Kagera mchuano ukifanyika Juni 25 kwenye Uwanja wa Kaitaba.


Edith alisema, mkoani Shinyanga mchuano utafanyika Juni 28, kwenye viwanja vya Chuo cha Biashara (SHYCOM) na mkoani Mara ikirindima Julai 2, kwenye Bwalo la Magereza  kabla ya fainali itakayofanyika Julai 9, kwenye Uwanja wa Kirumba.


Edith alisema, maaboresho ya michuano hiyo mwaka huu yamefanyika ikiwa ni pamoja na zawadi za washindi  kuliko mwaka jana, ili kuongeza mvuto na ushindani zaidi.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages