Breaking News

Your Ad Spot

Jun 19, 2011

UKOSEFU FEDHA ZA KUTOSHA KUGHARAMIA MIRADI YA MAENDELEO NI CHANGAMOTO KUBWA KWA UKUAJI WA UCHUMI NA MAENDELEO AFRIKA: KIKWETE

Rais Kikwete akiwa kwenye mkutano huo leo
 NA MWANDISHI MAALUM, KUALA LUMPUR, MALAYSIA
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amesema kuwa changamoto kubwa inayokwamisha ukuaji wa kasi zaidi wa chumi na maendeleo ya kasi zaidi ya Bara la Afrika ni ukosefu wa fedha za kutosha kugharimia miradi ya maendeleo. 
Taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, aliyeko Kuala Lumpur, imemkariri, Rais Kikwete  akisema kuwa kutokana ukweli kwamba njia za jadi za kupata fedha za kutosha za kuharakisha ukuaji wa kasi zaidi hazina uwezo wa kutoa fedha za kutosha kwa ajili ya maendeleo ni lazima nchi za Afrika zitafute namna nyingine mpya ya ubunifu zaidi ya kugarimia maendeleo ya Bara hilo na watu wake. 
“Changamoto siyo ukosefu wa miradi ya maana na inayotekelezeka ya maendeleo, bali tatizo ni ukosefu wa fedha za kutosha kugharimia miradi ambayo inaweza kuzitoa nchi za Afrika na watu wake katika umasikini kwa haraka zaidi,” Rais Kikwete amesema leo, Jumapili, Juni 19, 2011, mjini Kuala Lumpur, Malaysia.
 Rais Kikwete alikuwa anazungumza kwenye siku ya kwanza ya mkutano wa kimataifa wa mwaka huu wa Taasisi ya Smart Partnership Dialogue ambao pia unajulikana kama Langkawi International Dialogue 2011 ulioanzishwa rasmi mwaka 1995.
Shabaha kuu ya Smart Partnership ama Langkawi International Dialogue ni kufanya majadiliano ya kimataifa ya jinsi ya kuharakisha maendeleo duniani. Mada kuu ya mkutano wa mwaka huu ni “Enhancing Smart Partnership for Socio-Econimic Transformation”.

Akishiriki katika mjadala huo, Rais Kikwete amewaambia mamia ya washiriki kuwa changamoto na tatizo kubwa linalokwamisha ukuaji wa kasi zaidi wa uchumi na maendeleo ya kasi zaidi katika Afrika ni ukosefu wa fedha za maendeleo iwe ni kwa sekta binafsi ama sekta ya umma ama hata kwa Serikali.

Rais amesema kuwa chanzo kikuu cha fedha za maendeleo kwa nchi masikini za Afrika imekuwa ni kutokana na misaada ya maendeleo (ODA) lakini siku hizo hata hizo fedha za ODA zinapungua na wakati mwingine hazina uhakika wa kupatikana.

“Hata ukitofautiana na kampuni yenye asili ya nchi inayotoa misaada basi utanyimwa misaada hata kama kampuni yenyewe ndiyo yenye makosa,” amesema Rais Kikwete huku akishangiliwa na wasikilizaji wake.

Rais amesema kuwa wakati inakuwa vigumu kuvutia fedha za maendeleo kutoka nje, inakuwa vile vile vigumu zaidi kupata hata fedha kutoka vyanzo vya ndani. “Hakuna fedha za kutosha kwenye masoko ya fedha ya ndani na hivyo msingi mzima wa kifedha ni dhaifu sana. Msingi wa fedha wa ndani ni dhaifu na hata msingi wa fedha za kigeni wa nchi zetu ni masikini,”

Rais amesema kuwa hali hiyo inazifanya nchi za Afrika kujikuta katika wakati mgumu wa kushindwa kutimiza wajibu na majukumu yake katika kuwaletea wananchi maendeleo.

 “Hivyo, sisi katika Afrika tunahitaji kutafuta na kuangalia njia nyingine za ubunifu zaidi za jinsi ya kupata fedha za maendeleo, “ amesema Rais Kikwete na kuzitaka njia hizo kama vile ushirikiano kati ya sekta ya umma na ile ya binafsi (PPP), mikopo ya kushirikisha zaidi ya benki moja, mikopo kutokana na taasisi za fedha zinazokopesha fedha za maendeleo ya kijamii, ukopaji wa vyombo vya kufanyika kazi badala ya fedha taslim, njia za mikopo zinazodhaminiwa na Serikali, kuuza dhamana za kimataifa, na kukopa fedha kwenye masoko ya fedha.

Mapema mkutano huo ulifunguliwa na Waziri Mkuu wa Malaysia, Dato’ Sri Mohammed Najib Tun Abdul Razak ambaye hotuba yake ilizungumza masuala mengi na changamoto nyingi zinazoikabili dunia kwa sasa pamoja na umuhimu wa ushirikiano baina ya nchi zinazoendelea.  

1 comment:

  1. `Ukosefu wa pesa..' Kwanini kwasababu hatuuzi nje, au sio...tuna malighafi, hasa kutoka kutoka ardhini, madini, nk...lakini hatuna viwanda mama...tunauza kwa bei ndogo, wenzetu wanachukua malighafi hiyo wanaitengeneza wanakuja kutuuzia vipuri nk, kwa baei kubwa....oooh,
    Hatuwezi kuwa na viwanda mama, hatuwezi ku...ku...nashindwa hata kufikiri!

    ReplyDelete

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages