Breaking News

Your Ad Spot

Jun 1, 2011

ZIARA YA NAPE, MWIGULU RUKWA

KATIBU wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, akihutubia maelfu ya wananchi katika Uwanja wa Mandela mjini Sumbawanga, jana, siku ya kwanza ya ziara yake na Mjumbe wa NEC, Uchumi na Fedha, Mwigulu Nchemba, mkoani Rukwa 
Waliokuwa wanachama wa CHADEMA wakimpa kadi zao, Katibu wa NEC ya CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, katika mkutano wa hadhara uliofanyika, jana, katika Uwanja wa Mandela mjini Sumbawanga. Zaidi ya wanachama 50 wa CHADEMA walirudisha kadi zao na kujiunga na CCM 
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi CCM, Nape Nnauye akimkabidhi kadi mwanachama mpya wa CCM, Theresia Mwanakatwe, katika mkutano wa hadhara uliofanyika juzi, jana katika mji mdogo wa Laela, wilayani mkoani  Rukwa. Jumla ya wanachama wapya 82, waliojiunga na CCM walikabidhiwa kadi. Wapili kulia ni Katibu wa NEC, Uchumi na Fedha Nchemba Mwigulu.  
KATIBU wa NEC, Uchumi na Fedha CCM, Nchemba Mwigulu akikabidhi kwa Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye kadi za wanachama kutoka vyama vya upinzani ambazo wanachama wa vyama hivyo walimkabidhi baada ya kutangaza kuhama vyama vyao na kujiunga na CCM katika mkutano wa hadhara uliofanyika jana, katika Uwanja wa Mandela, mjini Sumbawanga. Mbali na CUF na NCCR-Mageuzi, Chadema pekee walihama 51. 
MKAZI wa kijiji cha Ntendo, Zakaria Lusambo akimshukuru, Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi CCM, Nape Nnauye baada ya kukabidhiwa baiskeli ya miguu mitatu pamoja na wenzake wanne wenye ulemavu wa miguu, wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika jana, kwenye Uwanja wa Mandela mjini Sumbawanga. Baiskeli hizo zimetolewa na Mbunge wa Sumbawanga, Aeshi Hilary (kushoto) 
KATIBU wa NEC, Itikadi na Uenezi CCM, Nape Nnauye na Katibu wa NEC Uchumi na Fedha CCM, Nchemba Mwigulu wakipatiwa maelezo na mmoja wa wasimamizi wa ujezi wa barabara yenye urefu wa kilometa 64 kati ya  Ikana hadi Laela mkoani Rukwa, walipokagua mradi wa ujenzi wa barabara hiyo, jana wakiwa njiani kwenda mjini Sumbawanga. eneo hilo ni kati ya Kilometa 190 Kutoka Ikana hadi Sumbawanga mjini ambazo zimo katika ujenzi ili kuwa katika kiwango la lami 
Nape akihutubia mkutano wa hadhara katika mji mdogo wa Laela, Sumbawanga  jana 
Nape akimsalimia na kumpa zawadi mkazi wa mji mdogo wa Laela  mweneye ulemavu wa vioungo 
Watoto na vijana wakimzunguka Nape baada ya mkutano katika mji mdogo wa Laela 
Waendesha pikipiki wakisubiri kusindikiza msafara wa Nape na Mwigulu kuingia mjini Sumbawanga, jana 
Nape akiteta jambo na Mbunge wa zamani wa Nkwela Crisant Mzindakaya 
Napa akishiriki  kucheza ngoma na kina mama wa Laela 
Mmoa wa makada wa CCM, akisaidia kwenda hospitali baada ya kuumia wakati wa pilikapilika za mapokezi ya Nape nje kidogo ya mji wa Sumbawanga.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages