
"Nilipokabidhiwa kadi ya uanachama wa CCM nilisoma kutoka katika kadi hiyo kwamba 'Nitajielimisha kwa kadiri na uwezo wangu na kutumia elimu yangu kwa faida ya wote, sasa hatua hii ya leo ni katika jitihada zangu za kuhakikisha natimiza imani hiyo", alisema Nape.
Alisema kuwa elimu aliyoipata atahakikisha anaitumia vilivyo kwa faida ya Watanzania wote hasa katika nafasi aliyomo sasa katika siasa.
Nape akijadili jambo na wahitimu wenzake wa Shahada ya Pili ya Uongozi wakati wa mahafali hayo. Kutoka kulia ni Meja Joseph Masanja, Magnus Mahenge na Zakia Omar
Nape akipongezwa na Mama yake wakati wa mahafali hayo
Watangazaji wa Chanel Ten nao wakaona lazima wampongeze Mheshimiwa Nape. Pichani, wakimpa zawadi maalum ya hongera nje ya ukumbi. Anayemkabidhi ni Fred Mwanjala na wengine ni Salama Hamad na Zainab Abdallah
Nape akipongezwa na Baba yake mdogo
Nape akiwa na wahitimu wenzake
Nape akiwa na wahitimu wenzake muda mfupi kabla yakutunukiwa shahada zao
Huyu jamaa ambaye ni Mkazi wa hesabu Ofisi ya Ukaguzi ya Taifa, Wilfred Gallaba, ghafla akamuona Nape, kumbe walikuwa wote kwenye mahafali hayo, naye pia amepiga nondozzz
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269