*Akagua na kuimarisha uhai wa Chama ngazi za chini kabisa za matawi na mashina. Ahudhuria vikao vya mashina na wajumbe wa nyumba kumi yaliyoko ndani ndani vijijini na kufanya mikutano ya hadhara iliyojaa shamra shamra, apokea wanachama wapya kibao
*Akagua hatua zinazoendelea katika upembuzi yakinifu wa mradi wa makaa ya mawe na chuma Liganga, aahidi wanannchi kushirikishwa kwa karibu mambo yakiiva.
UKAGUZI MWAMBAO WA ZIWA NYASA
KATIBU Mkuu wa CCM, Kanali mstaafu, Abdulrahman Kinana (wapili kulia) na Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye (kulia) wakiwa kwenye ufukwe wa ziwa Nyasa, kwenye mwambao wa ziwa hilo katika Kijiji cha Lupingu, Kata ya Lupingu Wilaya ya Ludewa mkoa wa Njombe, leo Mei 29, 2013, akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya Chama na kusikiliza kero za wananchi katika mkoa huo. Wengine ni Mbunge wa Ludewa, Deo Philikunjombe na Mbunge wa Mwibala Kange Lugora.
KATIBU Mkuu wa CCM, Kanali mstaafu, Abdulrahman Kinana (wapili kulia) na Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye (kulia) wakiwa kwenye ufukwe wa ziwa Nyasa, kwenye mwambao wa ziwa hilo katika Kijiji cha Lupingu, Kata ya Lupingu Wilaya ya Ludewa mkoa wa Njombe, leo Mei 29, 2013, akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya Chama na kusikiliza kero za wananchi katika mkoa huo.
Nape na Lugora wakieleweshana jambo kuhusu ziwa hilo
Kinana na baadhi ya viongozi aliokuwa nao kwenye msafara wake wakiwa kwenye ufukwe wa ziwa hilo kwenye kijiji hicho, Majini ni Mbunge wa viti maalum na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Pindi Chana.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na Nape wakipiga picha ya pamoja na baadhi ya walioambatana nao kwenye msafara huo.
Monica Msemwa akimuogesha mtoto kwenye ufukwe wa ziwa hilo la Nyasa. katika kijiji cha Lupingu wilayani Ludewa mkoani Njomba.
Kinana na msafara wake wakipita kwenye mitaa ya kijiji hicho cha Lupingu baada ya kukagua ufukwe wa ziwa Nyasa. (Pichzote na BASHIR NKOROMO)
KUKAGUA NA KUIMARISHA UHAI WA CHAMA NGAZI ZA CHINI KABISA
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akizungumza katika kikao cha shila namba moja, tawi la Lupingu, Wilaya ya Ludewa. Kushoto ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Pindi Chana, Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Njombe Deo Sanga au 'Jah People'
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimsalimia mwananchi aliyekuwa kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Kijiji cha wavuvi cha Lupingu, wilayani Ludewa
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimpa kadi ya uanachama wa CCM, Flowin Mkinga, katika mkutano mkubwa wa hadhara uliofanyika Kijiji cha Lupingu. Jumla ya wanachama wapya 32 walipata kadi za CCM.
Wanachama wapya waliopewa kadi wakila kiapo. Kulia ni Kinana akishiriki kwenye kiapo hicho cha utii kwa CCM
Msanii akiikung'uta ngoma kwa maarifa yake yote, wakati kikundi cha ngoma ya mng'anda kilipotumbuiza kwenye mkutano wa hadhara wa CCM uliofanyika kijiji cha Lupingu.
Wasanii wa ngoma ya mng'anda wakionyesha uhodari bwa kucheza ngoma hiyo, kwneye mkutano wa hatadhara uliofanyika katika kijiji cha Lupingu. (Picha zote na BASHIR NKOROMO
- MCHUCHUMA
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (wapili kulia) akionyeshwa sampuli mbalimbali za madini ya chuma kwenye kituo kinachofanya utafiti wa awali kuhusu kiwango cha chuma kinachoweza kupatikana kwa kuchimbwa eneo la Liganga, wilayani Ludewa mkoani Njombe alipotembelea karakana ya kampuni ya Kichina ya Tanzania China International Mineral Resorce Ltd, inayofanya uchunguzi huo. Anayempa maelezo ni Meneja Utawala wa kampuni hiyo, Tao Jian.
Tao Jian akiwaonyesha Kinana na msafara wake, ramani linalofanyiwa kazi na kampuni yake katika kutafiti aina na kiasi cha Chuma kitakachoweza kupatikana Liganga
Mabosi wa Kampuni ya Kichina inayofanya utafiti wa aina na kiasi cha chuma kitakachopatikana Liganga, wakitoa maelezo ya jumla kuhusu mradi huo unavyoendelea
Kilima cha madini ya Chuma, kinavyoonekana kwa mbali eneo la Liganga PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269