Na Elizabeth
John
BARAZA la Sanaa la Taifa (BASATA) kwa
kushirikiana na Chama cha Waandishi wa Habari za Sanaa na Utamaduni (CAJAtz), kesho
wanatarajia kuzikutanisha
taasisi mbalimbali
zinazohusika na urasimishaji ili
kutoa elimu kwa wasanii,
wadau na wakuzaji wa sanaa.
Akizungumza jijini Dar es Salaam, Kaimu katibu mkuu mtendaji
wa BASATA, Godfrey
Mngereza, alisema kuwa
taasisi hizo zitakutana katika ukumbi wa BASATA ulioko Ilala Sharif Shamba.
Mngereza alizitaja taasisi hizo ambazo zitakutana kuwa ni Bodi ya Filamu na Michezo ya Kuigiza, Chama
cha Hakimiliki na Hakishiriki Tanzania (COSOTA), Mamlaka
ya Mapato Tanzania (TRA) na Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA).
Alisema katika kuelekea urasimishaji wa sekta ya filamu na muziki ambao ulianza rasmi Januari mosi na ifikapo Julai
mosi mwaka huu hakuna kazi yoyote ya filamu na muziki itakayoingia sokoni bila kuwa na stampu
ya TRA.
Pia aliwataka wadau wa sekta ya
sanaa kupeleka
michango na hoja zao ili kuleta mustakabali utakaojenga
sekta ya sanaa.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269