OYEEEE!, KATIBU Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akihutubia mamia ya wananchi baada ya kufungua tawi la CCM la Kitongoji cha Wangamiko, Kata ya Malangali wilaya ya Wanging'ombe, Machi 31, 2013, akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji ilani ya Chama, na pia kukagua na kuimarisha uhai wa Chama katika mkoa wa Njombe.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akizungumza na wananchi kwenye Ofisi ya CCM mkoa wa Njombe leo Juni 1, 2013. Kushoto ni Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Njombe Deo Sanga.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akizindua jiwe la msingi Ujenzi wa Ofisi ya CCM wilaya ya Makete mkoani Njombe, jana.
Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akiwa na wana-CCM shina la Mdasi, Makete, baada ya kuzuia kwa muda msafara wake akiwa njiani kwenda Wanging'ombe jana.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiwaslimia wananchi wa kijiji cha Makonga, baada ya kusimama kwa muda barabarani walikokuwa wananchi hao, akiwa njiani kwenda Wanging'ombe jana.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akishiriki kufyatua matofali kwa ajili ya ujenzi wa zahanati ya Kata ya Samaria, wilayani Wanging'ombe mkaoni Njombe jana.
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akishiriki kufyatua matofali kwa ajili ya ujenzi wa zahanati ya Kata ya Samaria, wilayani Wanging'ombe mkaoni Njombe jana.
Wananchi wakiwa wamefurika nje ya Ofisi ya CCM, wilaya ya Wanging'ombe kumlaki Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye (waliopo chini ya bendera) baada ya kuwasili kwenye ofisi hiyo jana.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akizindua mradi wa mizinga ya nyuki, wa Jumuia ya Wazazi Kata ya Mlangali, wilaya ya Wanging'ombe mkoani Njombe, Machi 31, 2013. Mradi huo umeanza na mizinga 20.
Kinana akikagua moja ya mzinga wa nyuki wa mradi huo
Wananchi wakiwa kwenye Ofisi ya CCM ya Kitongoji cha Wangaiko, Njombe, wakati wa uzinduzi wa tawi hilo, uliofanywa na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, jana.
Wananchi wakimsindikiza kwa ngoma Kinana (kushoto) baada ya kuzindua tawi hilo
Kijana Joseph Kihongo Kijana ambaye alikuwa Kada wa Chadema, akionyesha kadi yake ya uanachama wa chama hicho kabla ya kuikabidhi kwa Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana (kulia), baada ya kuamua kuhamia CCM, katika mkutano wa CCM uliofanyika Machi 31, 2013, kwenye tawi la CCM Wangamiko, wilaya ya Wanging'ombe mkoani Njombe. Katika tukio hilo Kijana huyo na wanachama wengine wapya 150, walipatiwa kadi za CCM kwenye mkutano huo.
Your Ad Spot
Jun 1, 2013
Home
Unlabelled
TASWIRA MBALIMBALI, ZIARA YA KINANA MKOANI NJOMBE
TASWIRA MBALIMBALI, ZIARA YA KINANA MKOANI NJOMBE
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Top Ad
Your Ad Spot
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269