NAPE NNAUYE |
Kamati Kuu ya CCM Taifa itakutana ksho tarehe 23.8.2013 mjini Dodoma, chini ya Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete.
Kikao hicho cha Kamati Kuu kitafuatiwa na kingine cha siku mbili cha Halmashauri Kuu ya Taifa, kitakachoanza keshokutwa asubuhi..
Akizungumza leo mjini Dodoma, Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye amesema ajenda Kuu ya Kamati Kuu itakuwa kujadili maoni ya wana CCM juu ya rasimu ya Katiba.
Alisema hadi sasa CCM na wanachama wake wameshirikiana vya kutosha kwa kuzingatia sheria na taratibu zilizowekwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba.
Pia Kikao hicho kitajadili hali ya kisiasa na hatma ya madiwani Bukoba na Masuala Utumishi
Alisema siku ya Jumamosi asubuhi tarehe 24,kutakuwa na sherehe fupi za kuzindua Baraza la Ushauri la Wazee wa CCM kabla ya kikao cha halmashauri.
Baraza hilo linaundwa na Wenyeviti na Makamu Wenyeviti wastaafu wote wa CCM Taifa.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269