Breaking News

Your Ad Spot

Aug 23, 2013

MWENYEKITI WA CCM, RAIS JAKAYA KIKWETE WASILI DODOMA, AONGOZA KIKAO CHA KAMATI KUU YA CCM

 Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwapungia mkono Viongozi na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi waliofika kumlaki alipowasili Uwanja wa Ndege mjini Dodoma kwa ajili ya kuongoza kikao cha Kamati Kuu ya CCM, leo.
 Mwenyekiti wa CCM Taifa ,Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Katibu Mkuu wa CCM, Ndugu Abdulrahman Kinana uwanja wa Ndege mjini Dodoma.
 Mwenyekiti wa CCM Taifa ,Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dodoma na Mjumbe wa Kamati Kuu Ndugu Adam Kimbisa.

 Mwenyekiti wa CCM Taifa , Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana Ndugu Khamis Sadifa Juma.

 Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na mtumishi wa Chama Cha Mapinduzi  ndugu Octavian Kimario .
 Watumishi na wanachama wa Chama cha Mapinduzi wakishangilia kwa furaha ujio wa Mwenyekiti wa CCM Taifa , Rais Jakaya Mrisho Kikwete mara tu alipowasili Dodoma tayari kwa Mkutano wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu Taifa ya Chama.


 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akibadilishina mawazo na Mjumbe wa Kamati Kuu Ndugu Stephen Wassira kabla ya Kikao cha Kamati kuu kuanza leo Dodoma kwenye Ukumbi wa NEC.
 Wajumbe wa Kamati Kuu wakijadiliana jambo ndani ya ukumbi wa NEC kabla ya kuanza kwa kikao cha Kamati Kuu, Dodoma 23 Agosti 2013.
 Mjumbe wa NEC, Prof. Anna Tibaijuka akipitia Katiba ya Chama kabla ya kuanza kwa Kikao cha Kamati Kuu ndani ya ukumbi wa NEC.
Mwenyekiti wa CCM Taifa,Rais Jakaya Mrisho Kikwete ,akifungua kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri kuu ya Taifa CCM,Kushoto kwake ni Makamu wa CCM Zanzibar Ali Mohamed Shein na kulia ni Katibu Mkuu wa CCM ndugu Abdulrahman Kinana.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages