RAIS KIKWETE |
NA IMMACULATE MAKILIKA, MAELEZO
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya
Mrisho Kikwete ametunuku hati Idhini kwa vyuo vikuu na vyuo vishiriki viane baada ya
vyuo hivyo kutimiza taratibu zote za uanzishwaji wake hapa nchini.
Vyuo vilivyotunukiwa hati baada ya kutimiza taratibu zote ni Chuo Kikuu
cha Tumaini(TUMA),Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agustino (SAUT),Chuo Kikuu Kishiriki cha Ruaha(RUCo),Chuo Kikuu cha Mount Meru(MMU),pamoja na Chuo Kikuu cha
Arusha (UoA).
Vyuo vingine vilivyotunukiwa hati hiyo ni Chuo Kikuu
Kishiriki cha Tumaini Dar es salaam(TUDARCo) ,Taasisi ya Afrika ya Nelson
Mandela ya Sayansi na Teknolojia Arusha
(NM-AIST) na Chuo Kikuu cha Sayansi na
Teknolojia Mbeya(MUST).
Rais Kikwete
alivitunuku vyuo hivyo kwenye
hafla fupi iliyofanyika leo Ikulu
jijini Dar es Salaam , ambapo alisema
vimepiga hatua kubwa ya kuongeza
idadi ya wanafunzi wanaojiandikisha hadi kufikia laki moja sitini na sita elfu mwaka 2013
,ukilinganisha na idadi ya wanafunzi elfu arobaini ya mwaka 2005.
“Idadi kubwa ya
wanafunzi pekee haitoshi,ubora wa elimu uzingatiwe . Ikiwemo kupata wakufunzi
wengi na wenye sifa ni lazima sisi
wenyewe tuwekeze ndani ili kupata wakufunzi wakutosha katika vyuo vyetu ,”
alisema Rais Kikwete.
Aidha Rais Kikwete
alivitaka vyuo hivyo kutekeleza mkakati wa elimu wa Matokeo Makubwa Sasa (Big results now) ipasavyo
ili kuboresha elimu nchini kwa kuimarisha miundombinu ya vyuo vikuu nchini.
Aliongeza kuwa lazima viwe na mahitaji yote muhimu kwa kutoa
elimu bora ikiwemo vifaa vya kutosha,maabara,vyuo vya zamani viwekwe kwenye
viwango ili kukidhi utoaji wa elimu bora,
na kusisitiza vyuo vikuu vyetu vishirikiane na vyuo vikuu vya nje na kuvishauri vitafute vyanzo vingine vya mapato ili kukidhi uendeshaji badala ya kutegemea ada.
Utoaji wa
hati Idhini kwa vyuo vikuu ni zoezi
endelevu linalolenga kuboresha kiwango cha utoaji elimu ya juu nchini
ili kuwezesha wahitimu kukabiliana na changamoto za maendeleo
ya taifa letu kwa ujumla. Kwa mara ya mwisho zoezi hili lilifanyika tarehe 18 Agosti,2010 ambapo jumla ya vyuo
vikuu na vyuo vishiriki 13 vilitunukiwa
hati Idhini.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269