Breaking News

Your Ad Spot

Aug 23, 2013

RAIS JAKAYA KIKWETE KATIKA SHEREHE ZA KUAPISHWA RAIS MUGABE WA ZIMBABWE

Marais wastaafu Mzee Benjamin Mkapa na mkewe mama Anna Mkapa na Alhaj Ali Hassan Mwinyi wakiwa katika uwanja wa Taifa wa michezo wa Harare, Zimbabwe, katika sherehe za kuapishwa Rais Robert Gabriel Mugabe Agosti 22, 2013.

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimpongeza Rais Robert Gabriel Mugabe katika uwanja wa Taifa wa michezo wa Harare, Zimbabwe, katika sherehe za kuapishwa Rais huyo Agosti 22, 2013.
Rais wa Zimbabwe Mhe Robert Gabriel Mugabe akila kiapo katika uwanja wa Taifa wa michezo wa Harare, Zimbabwe, katika sherehe za kuapishwa kwake Agosti 22, 2013.


 Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete wakitoka katika uwanja wa Taifa wa michezo wa Harare, Zimbabwe, baada ya kuhudhuria sherehe za kuapishwa Rais Robert Gabriel Mugabe Agosti 22, 2013. Kulia ni Balozi wa Tanzania nchini zimbabwe, Mhe Adadi Rajabu

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages