DAR ES SALAAM, Tanzania
JESHI la Umoja wa Mataifa lililopo Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (MONUSCO) linafanya mipango kuuleta Tanzania mwili wa mwanajeshi wa Jeshi la wananchi wa Tanzania (JWTZ) Meja Khatib Mshindo aliyefariki dunia jana nchini DRC.
Taarifa iliyotolewa leo na Makao Makuu ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania imesema pia kwamba majeruhi walionusrika wakati Meja Mshindo na wenzake walipoangukiwa na bomu wakiwa katika eneo lao la ulinzi afya zao zinaendelea kuimarika wakati wakiendelea kupatiwa matibabu.
Taarifa Kamili ya JWTZ hii hapa
1. Kama
mnavyofahamu, JWTZ linashiriki katika operesheni za Umoja wa Mataifa huko Goma
DRC. Kikosi chetu kimeendelea kutekeleza majukumu yake ya kulinda amani kama
kinavyopangiwa na Jeshi la Umoja wa Mataifa nchini DRC lijulikanalo kama MONUSCO.
2. Tarehe 28 Agosti 2013 Wanajeshi wetu wakiwa
katika eneo lao la Ulinzi waliangukiwa na bomu katika eneo hilo na kusababisha
Majeruhi. Wakati wanapelekwa hospitali kwa matibabu, kwa bahati mbaya
mwanajeshi wetu mmoja, Meja Khatibu Mshindo alifariki dunia. Majeruhi wengine wanaendelea
na matibabu, na hali zao zinaendelea vizuri.
3. MONUSCO
inaandaa utaratibu wa kuleta mwili wa Marehemu.
Imetolewa
na:
Kurugenzi ya Habari na Uhusiano
Makao Makuu ya Jeshi.
Dar
es Salaam.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269