Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi
Dk.Ali Mohamed Shein,akisalimiana na Waziri wa Biashara za Nje na Ushirikiano
wa Kimataifa Nchini Uholanzi Bibi.Lilianne Ploumen,alipofika Ofisini kwake Mjini
The Hague jana akiwana ujumbe wake
katika ziara ya siku tano Nchini humo.[Picha na Ramadhan Othman,Uholanzi.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akibadilishana mawazo na Waziri wa Biashara za
Nje na Ushirikiano wa Kimataifa
Bibi.Lilianne Ploumen,nje ya Ofisi yake katika Mji wa The Hague Nchini
Uholanzi,akiwa katika ziara ya siku tano katika Mji huo. [Picha na Ramadhan
Othman,Uholanzi.]
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akisalimiana
na Kiongozi Mkuu wa Kampuni ya Mafuta ya Dutch Shell Peter Voser,alipofika
katika Makamo Makuu ya Kampuni hiyo katika Mji wa The Hague Nchini Uholanzi
jana akiwa katika ziara ya siku tano na ujumbe wake. [Picha na Ramadhan Othman,Uholanzi.]
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,(katikati) akifafanua jambo wakati wa mazungumzo kati ya Kampuni ya Mafuta ya Dutch Shell na Ujumbe wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, katika ukumbi wa Makao Makuu ya Kampuni hiyo Mjini The Hague nchini Uholanzi,(kutoka kulia) Waziri wa Ardhi, Maji Makaazi na Nishati Ramadhan Abdalla Shaaban, Kiongozi Mkuu wa Kampuni ya Mafuta ya Dutch Shell Peter Voser,(kushoto) Naibu Waziri wa Mambo ya Nje ya Nchi Mahadhi Juma Maalim, na John Crocker, ni miongozi mwa Viongozi wa Kampuni ya Shell. [Picha na Ramadhan Othman,Uholanzi.]
Rais wa Zanzibar
na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein, (kulia) na ujumbe wake wakiwa kwenye kikao cha pamoja na uongozi wa kampuni ya Mafuta ya Dutch Shell (Picha na Ramadhan Othman,Uholanzi.]
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269