Mkurugenzi
mkuu wa TANAPA Allan kijazi akiwahutubia wahitimu wa mafunzo ya
kuhifadhi maliasili katika chuo cha wanyama pori cha Mlele mkoani katavi
ambao hawapo pichani hapo juzi katika chuo cha wanyama pori cha mlele
ambapo wahitimu 96 walihitimu mafunzo ya awali ya wahifadhi wa
rasilimali za nchi na aliwataka wafanye kazi kwa uadilifu mkubwa ili
waweze kupambana na kutokomeza ujangiri na kuvunja mitandao ya majangiri
ya ndani ya nchi na nje ya nchi.
Askari
wa hifadhi ya mbuga ya wanyama (TANAPA) wakiwa wamesimama
wakimsikiliza mkurugenzi mkuu wa TANAPA ambaye hayuko pichani wakati
akifunga mafunzo ya askari hao waliohitimu mafunzo ya miezi 3 katika
chuo wanyama pori cha Mlele mkoa wa katavi namna ya kulinda rasilimali
za nchi ambapo amewataka wahitimu hao wafanye kazi kwa uaminifu
Askari wa hifadhi ya mbuga ya wanyama
(TANAPA) wakiwa wamekaa wakimsikiliza mkurugenzi mkuu wa TANAPA ALLAN
KIJAZI ambaye hayuko pichani wakati akifunga mafunzo ya askari hao
waliohitimu mafunzo ya miezi 3 katika chuo wanyama pori cha Mlele mkoa
wa katavi namna ya kulinda rasilimali za nchi ambapo amewataka wahitimu
hao wafanye kazi kwa uaminifu.
Picha na Katavi yetu Blog
*********************
Na Walter Mguluchuma wa Katavi yetu Blog.
Mpanda Katavi
Jumla ya
Askari 96 wa Shirika la Hifadhi la Taifa la Wanyama Pori (TANAPA) wametimu mafunzo
ya miezi mitatu katika
chuo kipya cha wanyama
pori cha Mlele kilichopo
Mkoa wa Katavi na kutoa
kiapo cha uti mbele ya Mkurugenzi
mkuu wa TANAPA Allan Kijazi
Askari hao wa TANAPA walimaliza mafunzo
hayo hapo juzi kwenye chuo
hicho cha wanyama Pori
cha Mlele akiwa ni mafunzo ya
kwanza hapa nchini
kwa TANAPA kutoa mafunzo kama hayo kwa Askari wa wanyama pori
kupatiwa mafunzo hayo kabla ya
kuanza kazi
Katika Risala yao ya
wahitimu wa mafunzo hayo ya
kulinda maliasili iliyosomwa na Bruno
Mbunda walieleza kuwa
wamejifundisha mbinu mbalimbali za
kulinda rasilimali za Taifa kwa Vitendo
na nadharia
Waliyataja baadhi
ya mafunzo waliyoyapata kuwa ni namna ya kufanya doria , kukamata waharifu
kumpekua mharifu na kutotumia
nguvu sana katika kukamata mharifu
pamoja na pia wamejifundisha namna ya kutumia silaha
Walieleza katika kipindi hicho cha mafunzo
wahitimi hao walifanikiwa kukamata waharifu
hamsini wakati wakifanya
doria katika maeneo mbambali ya
Mbuga ya Katavi na kwenye mapori ya akiba ya Rukwa Lwafi
Wahitimu hao
walieleza kuwa mafunzo hayo
yaliwashirikisha Askari 99
lakini watatu kati yao
wameshindwa kuhitimu zikiwemo
sababu mbambali kama
utoro na utovu wa nidhamu hari ambayo ilfanya wahitimu waliomaliza kubaki 96 ambapo kati yao mwanamke ni mmoja
na wanaume ni 95
Kwa upande wake
mkuu wamapori ya akiba ya Rukwa Lwafi
Joseph Mbung’ombe alimweleza mkurugenzi mkuu wa TANAPA kuwa chuo hicho
kinakabiliwa na changamoto mbalimbali
Alizitaja
changamoto hizo kuwa ni ukosefu wa mawasiliano
na ubovu wa miundo mbinu ya barabaa na
upungufu wa magari pamoja
idadi ndogo ya washiriki wa
mafunzo kwa wanawake na ufinyu wa bajeti
Nae Mkurugenzi wa Hifadhi
na Ikolojia Martini Loibook alieleza kuwa mafunzo hayo walioyapata
yanaumuhimu sana hasa kutokana na changamoto zinazoikabili nchi yetu
inayokabiliwa na wimbi la ujangili
Pia Mkurugenzi
wa utumishi na utawalla
wa TANAPA Witnes Shoo aliwataka wahitimu hao kufanya kazi
kwa uaminifu kwa kujituma na
wawe na didamu na wasiwe na tabia ya kutow a siri za ofisi
Mkurugenzi
Mkuu wa TANAPA Allan Kijazi
aliwaasa wahitimu hao wahakikishe
wanafanya kazi zao kwa uaminifu
mkubwa hasa katika shughuli zao katika kupambana kukomesha ujangili
Aliwataka
kutojihusisha na masuala ya ujangiri na
badal awahakikishe wanafanya kazi za kupambana na mitandao ya ujangiri iliyopo
ndani ya nchi na nje ya nchi
Alisema wapo
baadhi ya watumishi wa TANAPA ambao wamekuwa sio waaminifu hivyo wahitimu hao
wahakikishe wanafanya kazi zao kwa uaminifu pasipo kueubuniwa na mtu yoyote
yule au watu
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269