TIMU YAUNDWA KUSAKA MUUAJI
TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI
KAMISHNA CHAGONJI |
Mnamo tarehe 26
Januari, 2014 majira ya saa 12.00 asubuhi huko katika kijiji cha Mogabiri
katika mkoa wa kipolisi Tarime Rorya, jambazi asiyefahamika kwa jina aliwaua
kwa risasi Zakaria Mwita Marwa miaka 28 na Erick Lucas Maranya miaka 24 baada
ya kukutana nao njiani.
Siku hiyohiyo, majiara
ya saa 4:00 usiku, katika kijiji hichohicho cha Mogabiri, jambazi huyo alimuua
Robert Kisiri miaka 45 baada ya kuvamia Grocery inayomilikiwa na Chacha Ryoba
na kumjeruhi mtu mwingine mmoja.
Tarehe 27 januari, 2014
majira ya 11:30 alfajiri katika kijiji cha Mugabiri, jambazi huyo alifanya
mauaji tena kwa kumpiga risasi David Mwasi Matiko miaka 39 na kumpora simu yake
aina ya Nokia. Katika tukio hilo, pia, alimjeruhi Machungu Nyamahemba miaka 19
ambaye bado amelazwa katika hospitali ya Tarime kwa Matibabu.
Siku hiyohiyo ya tarehe
27 Januari, 2014 majira ya saa 2:00 usiku katika kijiji cha Nkende, jambazi
huyo alimuua kwa kumpiga risasi Juma Marwa Nyaitara miaka 30. Baada ya kufanya
mauaji hayo, jambazi huyo aliwapora simu zao za mkononi Chacha Magige na Masero
Marigiri wote wa kijiji cha Nkende.
Usiku wa kuamkia tarehe
28 Januari, 2014, jambazi huyo aliendelea kuua watu wengine watatu ambao bado
majina yao hayajafahamika. Mtu mmoja alipigwa risasi wakati akiendesha pikipiki
katika kijiji cha Nkende na wengine wawili waliuawa baada ya kukutwa na jambazi
huyo wakiwa wanatengeneza gari lililokuwa limewaharibikia katika kijiji cha
Mogabiri.
Hadi sasa juhudi kubwa
za kumsaka jambazi huyo zinaendelea kufanyika na Jeshi la Polisi kwa
kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama pamoja na wananchi. Aidha,
mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Ernesti Mangu, ametuma timu maalum kutoka
makao makuu ya jeshi la Polisi inayohusisha kamisheni ya Oparesheni, Upelelezi
na Intelijensia kwenda kuongeza nguvu katika juhudi zinazofanyika na ngazi ya
mkoa kuhakikisha kwamba, jambazi huyo anakamatwa upesi ili kuondoa hofu kwa
wananchi.
Jeshi la Polisi nchini,
linatoa wito kwa wananchi wote kutoa ushirikiano ili jambazi huyo aweze
kukamatwa na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria haraka.
Mwananchi mwenye
taarifa za mhalifu huyo anaweza kutumia namba ya simu ifuatayo 0754 785557.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269