Sehemu ya wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Loyola wakiwa katika
maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Kike Shuleni hapo. Baadhi ya wageni waalikwa wakiwa pamoja na wanafunzi wa Shule ya
Sekondari ya Loyola wakiwa katika maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Kike Shuleni
hapo.
SHULE ya Sekondari ya
Loyola ya Jijini Dar es Salaam leo imeadhimisha Siku ya Mtoto wa Kike shuleni
hapo kwa kutoa semina mbalimbali kwa wanafunzi wa kike juu ya changamoto
zinazowakabili watoto wa kike na namna ya kukabiliana nazo hasa kwa wanafunzi
shuleni. Mada anuai zimetolewa kwa wanafunzi juu ya changamoto zinazowakabili
hasa katika kipindi hiki ambacho nchi zinazoendelea zinakabiliwa na changamoto
ya utandawazi. Miongoni mwa watoa mada waalikwa katika maadhimisho ya siku hiyo
ni Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) ambao walitoa mada anuai kwa wanafunzi juu
ya kukabiliana na changamoto zinazowakabili hasa kipindi hiki ambacho
wanahudhuria masomo yao.
Mgeni rasmi wa na
Mwakilishi kutoka Kituo cha Maendeleo ya Uchumi, Rukia Shauri akikata keki
maalumu ya kuchangisha fedha zinazowasaidia baadhi ya wanafunzi wanaokubwa na
matatizo ambayo familia zao hushindwa kuwasaidia
Baadhi ya wanafunzi wa kike
waliofanya vizuri katika mtihani wa kidato cha pili suleni hapo walizawadiwa
katika hafla hiyo. Mgeni rasmi wa na Mwakilishi kutoka Kituo cha Maendeleo ya
Uchumi, Rukia Shauri akimpa zawadi mmoja wa wanafunzi hao
Mgeni rasmi wa na
Mwakilishi kutoka Kituo cha Maendeleo ya Uchumi, Rukia Shauri akilishwa keki na
mmoja wa washiriki katika maadhimisho hayo
Mgeni rasmi wa na
Mwakilishi kutoka Kituo cha Maendeleo ya Uchumi, Rukia Shauri (kulia) akilishwa
keki na Mkufunzi Chuo cha Mafunzo ya Jinsia (GTI) cha TGNP, Rashida Shariff
kwenye hafla hiyo.
Wanafunzi wa Kidato cha
Tano Loyola, wakiwa kwenye foleni kwa ajili ya kulishwa keki ya uchangishaji
fedha kwenye hafla hiyo Chuo cha Mafunzo ya Jinsia (GTI) cha TGNP, Rashida Shariff kulia
akizungumza na vyombo vya habari kwenye maadhimisho hayo. Baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Loyola wakiwa
katika maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Kike Shuleni hapo.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269