Breaking News

Your Ad Spot

Feb 4, 2014

ZAIDI WA WATANZANIA 35,000 HUFARIKI KILA MWAKA KUTOKANA NA SARATANI

Na Magreth Kinabo, MAELEZO
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Seif Rashid   amesema   zaidi ya 35,000 hufariki dunia kila mwaka kutokana na ugonjwa wa saratani.

Kauli hiyo imetolewa leo na waziri   huyo wakati akitoa tamko kuhusu   Siku ya Saratani Duniani ambayo huadhimishwa  kila mwaka  Februari 4 kwenye ukumbi wa mikutano wa wizara hiyo.

Aidha Dk. Rashid katika kuaadhimisha siku kutoa upimaji   Februari 4 na 5, mwaka huu bure,   hivyo aliitaka jamii kujitokeza   mapema ili kupima ugonjwa huo. Alisema huduma   za  ugonjwa huo ni haki ya kila mtu  na matibabu yake ni bure.

“Hapa Tanzania  tatizo la Saratani limekuwa likiongezeka mwaka hadi mwaka. Kila mwaka jumla ya wagonjwa wapya wa Saratani 44,000 hugundulika na zaidi ya 35,000 hufariki kutokana na ugonjwa huu,” alisema Dk. Rashid.

 Aliongeza kuwa takwimu za Taasisi ya Saratani Ocean Road, zinaonyesha kwamba kila mwaka inapokea wagonjwa wapya wa Saratani 5,000. Wagonjwa hao wanakuja wakati Saratani ikiwa katika kiwango cha juu - yaani hatua ya 3 na 4; na inasababisha uponaji wake kuwa mgumu.

Kauli mbiu ya maahimisho ya siku ya Saratani kwa mwaka huu  ni “Kupunguza unyanyapaa na kuondoa dhana potofu kuhusu Saratani”.

Aidha Dk. Rashid alisema saratani inayoongoza hapa nchini kwa wanaume ni Saratani ya Kaposi na Saratani ya Tezi Dume imekuwa ikiongezeka , na wanawake, Saratani ya Shingo ya Kizazi.

 Serikali katika kuboresha imeanzisha huduma hizi katika Hospitali ya Bugando, baadae itaanzishwa katika Hospitali za Rufaa za KCMC na Mbeya.

 Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Saratani Ocean Road, Dk. Twalib Ngoma  alisema  utafiti   uliofanywa  unaonesha kuwa  tumbaku  huchangia  wagonjwa  wa saratani kwa asilimia 40 .

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages