Breaking News

Your Ad Spot

Apr 12, 2014

KINANA AMALIZA ZIARA YA SIKU TANO KIGOMA, AHUTUBIA AKILOWA KWA KWA MVUA KUBWA BAADA YA KUTEMBELEA KUMBUKUMBU YA DK. LIVISTONE UJIJI NA KUZUNGUMZA NA WAVUVI KIBIRIZI

 Muasisi wa TANU Mzee Masoud Mwinyi Chande akimkaribisha Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana kwenye mnara wa kumbukumbu ya eneo alilofanyia mikutano na nyumba alikofikia na kulala, Baba wa taifa Mwalimu Nyerere, katika eneo la Ujiji, wakati wa harakati za kudai Uhuru wa Tanzania, Kinana alipotembelea eneo hilo, leo mwishoni mwa ziara yake ya siku tano mkoani Kigoma, kukagua uhai wa Chama na Utekelezaji wa ilani ya Chama.
Muasisi wa TANU Mzee Masoud Mwinyi Chande akimkaribisha Kinana kwenye mnara wa kumbukumbu Nyererealikofanya mkutano  Ujiji wakati wa harakati za kudai Uhuru
 Kinana akizungumza na wananchi kwenye mnara huo wa kumbukumbu
 Kinana akiwa katika chumba alimolala Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere katika nyumba hiyo ya Ujiji
 Kinana akiruka mtaro baada ya  kutoka kwenye nyumba na mnara huo wa kumbukumbu
 Kinana (kushoto) akimsikiliza kwa makini Katibu wa CCM Kata ya Kasingirima, Ujiji, Amri Athuman wakati akisoma risala kuhusu ujenzi wa Jengo la Ofisi ya CCM ya Kata hiyo. na kueleza kwamba umaliziaji wa jenzi wa jengo hilo unahitaji kiasi cha sh. milioni 19 kwa kuwa ujenzi wa jengo hilo ulioanza zaidi ya miaka 30 iliyopita umeshindikana kumalizika hado sasa.
 Kinana akijibu risala hiyo, na kusema kwamba, haridhiki kuhusu kuzungumzia yeye kuchangia ukamilishaji wa jengo hilo, bila kujua kwa nini hadi sasa limeshidikana kuisha licha ya kujengwa tangu kabla ya mfumo wa vyama vingi nchini ambao ni zaidi ya miaka 30 sasa, huku akitia shaka kwamba huenda umangumeza na ubadhirifu wa viongozi waliokuwa madarakani umechangia ukwamishaji huo.
 Kinana akijadili jambo na Mbunge wa Kigoma mjini Peter Serukamba, wakati wakitoka kwenye jengo hilo

ATEMBELEA KUMBUKUMBU YA DK. LIVINGSTONE, UJIJI
Kinana akionyeshwa baadhi ya michoro ya kumbukumbu katika jumba la makumbushgo ya Livingstone alipotembelea makumbusho hayo yaliyopo Ujiji Kigoma
 Kinana akionyeshwa baadhi ya michoro ya kumbukumbu katika jumba la makumbushgo ya Livingstone alipotembelea makumbusho hayo yaliyopo Ujiji Kigoma
 Kinana akitazama mchoro unaonyeesha Dk. Livingstone na Kar Peter wakisalimiana baada ya kukutana eneo hilo la Ujiji ambalo hadi sasa linaitwa Livingstone.
 Kinana akionyeshwa eneo ilipojengwa kumbukumbu kuonyesha walipokutaba LIvingstone na Kar Peters
 Jiwe na msingi lenye kumbukumbu 
 Kinana akitona kwenye jengo hilo la makumbusho ya Dk. Livingstote
 Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akiwa na baadhi ya viongozi wa Kigoma, nje ya jengo la kumbukumbu ya Dk. Livingstone.
 KInana na msafara wake wakipita njia iliyotumiwa kusafirisha watumwa kutoka eneo hilo la Livingstone, Ujiji kwenda Tabora

ATEMBELEA NA KUSIKILIZA KERO ZA WAVUVI KIBIRIZI
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akizungumza na wavuvi wa aina mbalimbali katika ziwa Tanganyika, alipokutana nao kwenye kituo chao eneo la Kibirizi mkoani Kigoma  ili kufahamu kero zao na kujadiliana nao njia ya kuzimaliza.
Katibu Mkuu wa CCM, Kinana akifungua tawi la CCM Kibirizi

AHUTUBIA MKUTANO WA HADHARA HUKU AKIANDAMWA NA MVUA KUBWA
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akisalimia wananchi alipowasili Uwanja wa Mwanga Community Centre, kufanya mkutano wa hadhara leo
 Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye ambaye aliambatana na Kinana kwenye mkutano huo, akisalimia wananchi baada ya kuwasili
 Msanii wa ngoma ya Warumba kutoka Mwanga Katubuka, akitoa burudani wakati wa mkutano huo
 Kinana akifurahia jambo wakati wa mkutano huo. Kulia ni Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa, Kirumbe Ng'enda, na  kushoto ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Kigoma, Dk., Walid Kabourou
 Nape akihutubia mkutano huo
 Katibu wa Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akihutubia kwenye mkutano huo kwenye Uwanja wa Mwanga Community Centre, Kigoma huku mvua kubwa ikimwandama yeye na wananchi waliokuwa wakimsiliza kwa makini licha ya mvua hiyo.
 Wananchi waliokuwa kwenye mkutano huo wakijisiti mvua kwa mwavuli usiwatosha wote wakati wa mkutano huo
Baadhi ya vijana waliokuwa kwenye mkutano wakijinga mvua kwa mtandio. Picha zote na Bashir Nkoromo- theNkoromo Blog

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages