Mkufunzi wa Ngoma za Samba regge,
Manni Spaniol akimwelekeza mmoja wa watoto wanaoshiriki warsha ya fit
for life iliyoandaliwa na kituo cha Baba watoto cha Mburahati kwa Jongo,
Jijini Dar es Salaam.
Mkufunzi wa ndani, Mwajabu
Omari akimwelekeza namna ya kufanya sarakasi mmoja wa watoto
wanaoshirika kwenye warsha ya sarakasi na ngomba za samba regge
iliyoandaiwa na kituo cha Baba Watoto
Mafunzo ya Sarakasi
Wanafunzi
na wakufunzi wakifanya mazoezi ya kujiandaa na onyesho la muziki wa
samba regge litakalofanyika kesho kwenye viwanja vya Kasulu, Mburahati
kwa Jongo.
Watoto zaidi ya 80 kutoka kituo cha Baba Watoto kesho
wanatarajiwa kupanda katika jukwaa moja kuonyesha ngoma za kibrazili na
sarakasi ikiwa ni sehemu ya kuhitimisha mafunzo ya wiki tatu ya michezo hiyo kupitia
mradi wa fit for life yaliyokuwa yakifanyika Mburahati jijini Dar es Salaam.
Warsha hiyo ambayo imewashirikisha watoto walio kwenye mazingira magumu kati ya umri wa miaka 10 hadi 25 imefadhiliwa na umoja wa ulaya (EU) na kusimamiwa na kituo cha Utamaduni cha Ujerumani Goethe-Institut kwa ubia na Ufa-Fabrik ya Ujerumani na Parapanda Theatre.
Meneja mradi wa Fit for life, Habiba Issa amesema kuwa onyesho hilo linafanyika kesho Ijumaa kuanzia saa tisa mchana
kwenye kiwanja cha Kasulu Mburahati kwa Jongo, ambapo watoto hao wataonyesha ustadi
wa miruko ya sarakasi, trapezi na muziki wa samba regge kutoka nchini Brazil.
Alisema kuwa onyesho hilo litakuwa ndio hitimisha
la warsha ya wiki tatu ambayo ililega kuwajengea uwezo watoto na vijana wa
kufanya shughuli za sanaa ambazo ni pamoja na ushonaji wa maleba, muziki, ufundi
seremala, ujengaji wa majukwaa makubwa na taa na utaalamu wa sauti ya jukwaani.
“Tunategemea vijana hawa watatumia ujuzi huu katika
maisha yao ya kila siku maana mwaka jana waijifunza mengi na sasa tumewaongezea
uwezo zaidi ili kuwawezesha kujitegemea na kuinua uchumi wao na kuwapa mbinu
nyingi za kukabiliana na maisha” alisema Issa.
Akizungumzia maandalizi ya onyesho hilo Msimamizi
wa wakufunzi wa ndani katika mafunzo hayo, Mkude Kilosa alisema kuwa vijana
wako tayari kwa onyesho hilo na kwamba sasa wako katika hatua za mwisho za
maandalizi hayo.
“Mafunzo yanaendelea vizuri na sasa tunajiandaa na
onyesho letu la ijumaa ambapo wale waliojiunga nasi mapema wako katika hali
nzuri na sasa tunashughulika na hawa wapya ili waweze pia kufanya onyesho siku
hiyo” alisema Kilosa
Alisema kuwa mbali na kuwafundisha watoto hao namna
ya kucheza sarakasi na muziki wa samba regge pia wanawaandaa kuwa walimu wa
sanaa hizo ili waweze kuwafundisha wengine na kukuza vipaji vya watu wengi
zaidi nchini.
Alisema onyesho hilo linatarajiwa kuwa la kuvutia
kutokana ujuzi waliopata watoto hao kutoka kwa wakufunzi wao kutoka Ujerumani, Ufaransa
na Kambodia.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269