Mshauri wa Kimataifa wa Kujitegemea, James Rugemalira akifuatilia matukio mbalimbali kwenye semina hiyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mabibo Beer Wines and Spirits Limited, Benadicta Rugemalira, akiwa kwenye semina hiyo.
Daktari bingwa wa ugonjwa wa saratani ya matiti kutoka nchini India, Profesa Anthony Pais, akitoa mafunzo kuhusu ugonjwa huo kwa madaktari wa kitanzania na wadau mbaliombakli wa sekta ya afya. Semina hiyo ilifanyika Dar es Salaam jana, Hoteli ya Protea Courtyard Seaview.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mabibo Beer Wines and Spirits Limited, Benadicta Rugemalira, akizungumza katika semina hiyo. Kampuni hiyo ilidhamini semina hiyo.
Profesa Anthony Pais, akiwa na madaktari wa kitanzania. Kutoka kushoto ni Executive Chairman Tanzania Creative Industries Network (TACIN), Anic Kashasha na Dk.Paul Mareale.
Profesa Anthony Pais (kushoto), akielezea jambo kuhusu ugonjwa huo.
Mshauri wa Kimataifa wa Kujitegemea, James Rugemalira akiteta jambo na Mkurugenzi wa Kampuni ya Mabibo Beer wines and Spirits Limited, Benadicta Rugemalira.
Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) ,
Dk.Malina Njelekela(kulia), akizungumza na wadau mbalimbali katika semina hiyo.
Mshauri wa Kimataifa wa Kujitegemea, James Rugemalira akizungumza na waandishi wa habari. Kulia ni mke wake ambaye ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Mabibo Beer wines and Spirits Limited, Benedicta Rugemalira na Profesa Anthony Pais.
Profesa Pais (katikati), akiwa na wenyeji wake. Kutoka kulia ni Dk.Paul Mareale, James Rugemalira, Dk.Malina Njelekela na Benedicta Rugemalira.
Profesa Pais akizungumza na waandishi wa habari.
Mshauri wa Kimataifa wa Kujitegemea, James Rugemalira (kushoto), akipeana mkono na daktari bingwa wa ugonjwa wa saratani ya matiti kutoka India, Profesa Anthony Pais (kulia), baada ya kutoa mafunzo kwa madaktari wa Tanzania na wadau wa sekta ya afya kuhusu ugonjwa huo, Dar es Salaam jana. Katikati ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mabibo Beer Wines and Spirits Ltd, Benedicta Rugemalira, waliodhamini mafunzo hayo ya siku moja.
Profesa Pais (mwenye suti katikati), akiwa katika picha ya pamoja na wenyeji wake.
Profesa Pais (mwenye suti katikati), akiwa katika picha ya pamoja na wenyeji wake.
Wadau mbalimbali na maofisa wa Kampuni ya Mabibo wakiwa kwenye semina hiyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) ,
Dk.Malina Njelekela(kulia), akiteta jambo na viongozi wengine kwenye semina hiyo.
Profesa Pais akifurahia jambo na Executive Chairman Tanzania Creative Industries Network (TACIN), Anic Kashasha.
Wadau wakiwa kwenye semina hiyo. Kulia ni Mmoja wa Wakurugenzi wa Kampuni iliyokuwa ikifua umeme ya VIP, Joe Mgaya.
Wanahabari wakiwa kwenye semina hiyo.
wadau mbalimbali wakiwa kwenye semina hiyo.
Hali halisi ya ugonjwa wa saratani ya matiti inasikitisha sana.
Wadau wakiwa kwenye mkutano huo.
Mama Rugemalira na Dk.Njelekela wakifuatilia matukio mbalimbali katika semina hiyo.
Dk. Mareale na Kashasha wakiteja jambo kwenye semina hiyo.
Dk.Fred (kushoto), akiwa na wadau wengine katika semina hiyo.
Wageni waalikwa wakiwa kwenye semina hiyo.
Wadau hawa wakifuatilia kila tukio katika semina hiyo.
Hawa nao walikuwa makini kufuatilia kila jambo katika semina hiyo.
Wakina mama wakiwa wamepigwa butwaa na kushika tama baada ya kuona picha za matiti yenye saratani wakati zikioneshwa na Profesa Pais.
Profesa Pais akiwa na wenyeji wake.
Hapa maswali kuhusu ugonjwa huo yakiulizwa.
Mzee James Rugemalira akichangia kuelezea jambo.
Wadau wakichangia kueleza chochote kuhusu ugonjwa huo.
Washiriki wa semina hiyo wakifuatilia kila jambo.
James Rugemalira na mke wake wakimpongeza Dk. Njelekeza baada ya kutoa hutuba yake.
James Rugemalira(kulia), akisisitiza jambo.
Profesa Pais (mwenye suti katikati), akiwa katika picha ya pamoja na wenyeji wake. (Picha zote na Dotto Mwaibale wa mtandao wa www.habari za jamii.com na Philemon Solomon wa Full Shangwe)
Dotto
Mwaibale
ULAJI wa
nyama nyekundu imeelezwa uchangia kwa kiasi kikubwa kupatwa na ugonjwa wa
saratani ya matiti ambao umekuwa ni tishio duniani.
Hayo
yalibainishwa na Daktari bingwa wa
ugonjwa wa saratani ya matiti Profesa Anthony Pais kutoka Bangarole India
katika semina ya siku moja kwa madaktari wa Tanzania na wadau wa sekta ya afya
iliyofanyika Dar es Salaam juzi.
“Ulaji wa
nyama nyekundu na vyakula vyenye mafuta unachangia kwa kiasi kikubwa kupata
ugonjwa huo ambao umekuwa tishio duniani” alisema Pais.
Profesa
Pais alisema mfumo wa maisha wa kula vyakula bila mpangilio na kukosa kufanya
mazoezi pia ni moja ya sababu inayoweza kumsabishia mtu kupata ugonjwa huo.
“Ni muhimu
kujenga tabia ya kufanya mazoezi walau kwa dakika 20 kila siku itasaidia
kupunguza changamoto ya ugonjwa huo.
Akizungumzia
ugonjwa wa saratani ya matiti alisema hauwapati wanawake pekee bali na wanaume
lakini kutokana na kukuwa kwa teknojia mpya wamekuwa wakiutibu bila ya
kuliondoa titi lenye matatizo.
Alisema
hivi sasa dunia imekuwa ikitumia gharama kubwa kwa matibabu ya ugonjwa wa saratani huku vikifunguliwa vituo
vingi vya kutibu ugonjwa huo.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya
Muhimbili (MNH) , Dk.Malina Njelekela
alisema ni muhimu sasa kwa madaktari wa kitanzania kujifunza teknolojia hiyo ya
upasuaji wa saratani ya matiti bila ya kuliondoa titi husika.
Mshauri wa Kimataifa wa Kujitegemea James Rugemalira
ambaye amemleta Profesa huyo hapa nchini amesema baada ya kuona changamoto ya
ugonjwa huo aliona ni vema kumleta mtalaamu huyo ili kuona namna ya kusaidia.
Alisema
profesa huyo pamoja na kutoa mafunzo hayo mafupi pia atapata fursa ya
kutembelea mikoa kadhaa ya kanda ya kati ili kutoa uzoefu wake kuhusu ugonjwa
huo.
Kampuni ya
Mabibo Beer Wines and Spirits Ltd ilidhamini semina hiyo iliyofanyika Hoteli
nya Protea Courtyard kupitia vinywaji vyake vya Windhoek Draught na Windhoek
Lager.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269