Mkutano wa WHO kuhusu Ebola mjini Geneva.
Shirika la afya duniani WHO limesema kuwa
damu ya watu ambao wameponea ugonjwa wa Ebola inaweza kutumiwa
kuwauguza wagonjwa wengine.
Katika mkutano mjini Geneva, wataalam wa
shirika hilo walikubaliana kwamba hii itakuwa njia ya haraka na ilio
salama dhidi ya ugonjwa wa Ebola,sababu kuu ikiwa kwamba kinga ya mwili
katika damu ya mtu aliyepona inaweza kukabiliana na virusi hivyo.
Wataalam hao pia wanataka matibabu mengine kuharakishwa ikiwemo dawa ya Zmapp pamoja na chanjo zengine mbili.
Idadi ya watu wanaodaiwa kufariki kutokana na ugonjwa wa Ebola imepita elfu mbili. Zaidi ya watu elfu nne wameambukizwa ugonjwa huo huku tiba yake ikiwa bado haijajulikana. Chanzo: BBC
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269