Na
Frank Mvungi MAELEZO
Benki
Kuu ya Tanzania imetoa toleo jipya la sarafu ya shilingi 500 itakayoanza
kutumika Oktoba 2014 itakayokuwa mbadala wa Noti ya shilingi 500 inayoonekana kuchakaa
haraka.
Hayo
yamesemwa leo Jijini Dar es salaam na
Mkurugenzi wa Huduma za kibenki wa benki hiyo Bw. Emmanuel Boaz
wakati wa mkutano na waandishi wa habari.
“Noti
ya shilingi 500 hupita kwenye mikono ya watu wengi zidi na ndiyo inayotumika
zaidi kwenye manunuzi ya kawaida hivyo kuchakaa haraka ndio maana tumeamua
kutoa toleo la sarafu itakayoanza kutumika mapema mwezi wa 10 mwaka huu.”alisema
Boaz.
Akifafanua
zaidi Boaz amesema Sarafu hukaa kwenye mzunguko kwa miaka mingi zaidi kuliko
noti na pia noti zimekuwa zilikaa katika mzunguko kwa muda mrefu bila
kurejeshwa kwenye mabenki kwa wakati muafaka ili zibadilishwe.
Akitaja
sifa za sarafu hiyo mpya Boaz amesema kwanza umbo lake ni la duara lenye
michirizi pembezoni na kipenyo cha milimita 27.5 na uzito wa gramu 9.5.
Sifa
nyingineni kuwa ina rangi ya fedha na imetengenezwa kwa madini aina ya chuma na
Nickel na kwa upande wa mbele ina sura ya Rais wa kwanza wa Serikali ya
mapinduzi ya Zanzibar sheikh Abeid Aman Karume na kwa nyuma ina taswira ya
mnyama nyati akiwa mbugani.
Pia
Boaz alibainisha kuwa sarafu hiyo kwa upande wa
nyuma ina kivuli kilichojificha ambacho huonesha thamani ya sarafu ya
500 au neno BOT inapogeuzwa geuzwa.
Kwa
upande wa matumizi Boaz amesema sarafu hiyo itakapoanza kutumika itatumika
sambamba na noti za shilingi 500 hadi zitakapokwisha kwenye mzunguko.
Benki Kuu ya Tanzania ndiyo chombo chenye jukumu la
kutoa sarafu na noti halali (legal tender) zinazotumika nchini ambapo katika kutimiza jukumu hili
Benki kuu hutengeneza noti na sarafu zenye uwiano mzuri wa thamani
(denomination) unaozingatia uwezekano wa zile zenye thamani kubwa kuweza
kugawika katika zile zenye thamani ndogo.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269