Na Matukiodaima Blog
HALI ya kisiasa ndani ya chama cha Demokrasia na maendeleo (Chadema) mkoa wa Iringa si shwari baada ya mwenyekiti wake mkoa wa Iringa Mustapher Msowela kumfikisha polisi mwenyekiti wa chama hicho wilaya ya Iringa mjini, Frank Nyalusi
HALI ya kisiasa ndani ya chama cha Demokrasia na maendeleo (Chadema) mkoa wa Iringa si shwari baada ya mwenyekiti wake mkoa wa Iringa Mustapher Msowela kumfikisha polisi mwenyekiti wa chama hicho wilaya ya Iringa mjini, Frank Nyalusi
Nyalusi
ambae pia ni diwani wa kata ya Mvinjeni jimbo la Iringa mjini juzi
alitiwa nguvuni na jeshi la Polisi kabla ya kuachiwa kwa dhamana.
Nyalusi
aliyeshitakiwa katika kituo cha Polisi cha kati cha mjini Iringa jana, anatuhumiwa
kumtusi mwenyekiti wake huyo wa mkoa kupitia mitandao ya simu; matusi
yanayoendelea kuchunguzwa na jeshi hilo.
Nyalusi
amekamatwa kwa tuhuma hiyo ikiwa ni siku chache tu baada ya kudaiwa kutoa
tuhuma za uongo kwa lengo la kujipatia umaarufu dhidi ya mfanyabiashara maarufu
wa mjini Iringa, Salim Asas ambaye pia ni Kamanda wa Umoja wa Vijana wa Chama
cha Mapinduzi (UVCCM) mkoa wa Iringa.
Katika
mkutano wa hadhara uliofanywa na Chadema Desemba 21 kwenye uwanja wa
Mwembetogwa mjini Iringa, Nyalusi ambaye pia ni diwani wa kata ya Mivinjeni
alitoa tuhuma zinazowahusisha vijana watatu ambao hata hivyo hakuwataja majina
kwamba walitumwa na Asas kwenda kumuua.
Asas
kwa kupitia kwa wakili wake, Alfred Kingwe amekanusha tuhuma hizo alizoziita ni
za kipuuzi ambazo haziwezi kubebeka hata kwa mzani mdogo wa kupimia madini.
Ili
kumsafisha mteja wake, Kingwe alisema ndani ya siku 14 toka akabidhiwe hati ya
madai (Demand Note), Nyalusi anatakiwa kuitisha mkutano katika eneo lile lile
alilotolea tuhuma hizo na kuzikanusha vinginevyo atafikishwa mahakamani.
Akizungumza
na wanahabari jana, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Iringa, Ramadhani Mungi
alisema; “Kuhusu tukio la kumtukana
mwenyekiti wake wa mkoa, Nyalusi alikamatwa jana mara baada ya Msowela
kuwasilisha malalamiko yake polisi, akahojiwa na kuachiwa baada ya kukamilisha
taratibu za dhamana.”
Alisema
jeshi la Polisi linaendelea kuchunguza tukio hilo la kijinai na endapo litathibitika
kuwa la kweli, Nyalusi ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Mivinjeni mjini Iringa
atafikishwa mahakamani.
Kuhusu
tukio linalomuhusisha na Asas, Kamanda Mungi alisema jeshi la Polisi limefanya
mahojiano ya awali na wahusika hao.
“Jambo
hili lipo, tunachunguza; yapo maneno Nyalusi ameyatamka kwenye mkutano wao wa hadhara
kwamba ametishiwa kuuawa, ametumiwa watu watatu kwenda kumuua wakiwa na visu. Kumtishia
mtu ni kosa la jinai na kumtuma mtu kwenda kumdhuru mtu mwingine ni kosa la
jinai, kwahiyo tunachunguza” alisema.
Alisema
katika mazingira ya uwazi, Polisi inachunguza suala hilo ili kujua Nyalusi
alitishiwa katika mazingira gani; alitishiwa na nani na kwanini hakwenda kutoa
taarifa hiyo Polisi na kufungua kesi ili Polisi iwakamate wahusika na kulinda maisha
yake.
“Lakini
tunajaribu kuangalia kama hakutishiwa na ametamka vile katika mkutano wa
hadhara, lengo lake lilikuwa ni nini na kama anajua madhara yake kwa jamii
iliyosikia taarifa hiyo ni yepi,” alisema.
Alisema
kama itabainika taarifa zilizotolewa na Nyalusi ni za uongo, sheria itachukua
mkondo wake na kama itadhihiri ni za kweli sheria pia itachukua mkondo wake.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269